Chama tawala China chaidhinisha "rais wa maisha"

Xi Jinping walking in front of delegates' tables and empty chairs Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023

Chama tawala cha National People's Congress nchini China, kimeidhinisha marekebisho ya kipengee cha katiba, ya kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.

Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.

Wakosoaji wameonya kuhusiana na hatari ya kuondoa muda wa mihula miwili ya uongozi wa Rais, ambayo ililetwa na Deng Xiaoping mwaka 1982.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hatua hiyo sasa imemfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023

Chama hicho kinasema kuwa, mabadiliko hayo yataupa nguvu na kuboresha mfumo wa uongozi nchini humo.

Yeyote anayepinga mabadiliko hayo, kwa hofu kuwa itampa nguvu zaidi mtu mmoja, amezimwa nchini humo.

Waandishi habari walinyimwa idhini ya kuingia Bungeni, kushuhudia zoezi hilo la kupiga kura likifanyika.

Mada zinazohusiana