Urusi yafanyia majaribio kombora lisiloweza kuzuiwa

missile with streak of light behind it Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kombora la Kinzhal linaelezwa kuwa linaweza kusafiri mara kumi ya kasi ya sauti na linaweza kufika hadi kilomita 2,000

Urusi inasema kuwa imefanakiwa kulifanyia majaribio kombora lake lisiloweza kuzuiwa, moja ya makombora yaliyotangawa na Rais Vladimir Putin mapema mwezi huu.

Wizara wa ulinzi ya Urusi ilichapisha video ikionyesha kombora hilo likifyatuliwa kutoka kwa ndege ya vita na kuacha moshi nyuma.

Ilisema 'lengo' la kombora hilo liligongwa.

Tarehe mosi mwezi huu , Rai Putin alitangaza kuwa kombora la Kinzhal na la kiwango cha juu.

Kombora la Kinzhal linaelezewa kuwa linaweza kusafiri mara kumi ya kasi ya sauti na linaweza kufika hadi kilomita 2,000.

Wizara ya ulinzi ilisema kuwa kombora hilo lilifyatuliwa kutoka kwa ndege aina ya MiG-31 ambayo ilipaa kutoka uwanja ulio kusini magharibi mwa Urusi siku ya Jumamosi.

"Uzinduzi huo ulienda kulingana na mpango, kombora hilo liligonga lengo lake," wizara ilisema.

Putin anatarajiwa kuchaguliwa tena kama rais wa Urusi wiki moja inayokuja.

Kama sehemu ya hotuba yake kwa taifa ya tarehe mosi mwezi hu, alicheza kanda ya video ambayo ilionekana kuonyesha mvua wa makombora katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Marekani ilijibu ikisema kwa hiyo haistahili kuwa taibia ya taifa kama Urusi.

Mada zinazohusiana