Mkutano wa Trump na Kim Jong-Un waanza kuandaliwa

Mkutano huo unatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa dunia
Image caption Mkutano huo unatajwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa dunia

Ujumbe wa Korea Kusini upo katika jitihada za maandalizi ya mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Viongozi hao wa Korea kusini wanatarajiwa kufika China na Japan kutoa maelezo juu ya mkutano huo.

Muda na mahali pa kufanyika mkutano huo bado haijajulikana.

Image caption Trump amesema anatarajia watafikia muafaka mzuri

Viongozi wa juu wa Korea Kusini wiki iliyopita walifikisha ujumbe kwa Rais wa Marekan Donald Trump juu ya kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, huku Trump akikubali mara moja kushiriki katika mkutano huo na kuwapa taarifa china na mshirika wake Japan mara baada ya kupokea taarifa hizo.

China imeonesha nia ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo lakini mahala pengine pa kufanyika mkutano huo pametajwa kuwa huenda ikawa ni uswizi, Sweden ama Panmunjom.

Wakati huo huo viongozi wa usalama Nchini marekani wamesema kuwa wanajua hatari iliyoko katika mkutano huo lakini wamefurahishwa na hatua ya Trump kukubali kushiriki.

Image caption Suala la makombora ya nyuklia linatajwa kuwa ajenda muhimu ya mazungumzo

Mkurugenzi wa CIA Mike Pompeo amesema kuwa, anajua ugumu wa kujihusisha na Korea kaskazini, lakini ana amini kuwa Trump amekubali kushiriki mazungumzo hayo kwa ajili ya kuondoa matatizo na korea kaskazini na si vinginezvyo.

''Hiki ni kitu ambacho kimepiganiwa kwa miongo kadhaa sasa, na wakati huo huo amekubali kuzungumza juu ya mpango wa kusitisha Nuklia, mwisho itajulikana kuwa sio maneno tuu au nani amesema nini, uongozi huu uko makini na wakati wote wa mazungumzo shinikizo juu ya korea kaskazini liendelea , hakuna kumpuzika hadi rais ahakikishe kuwa amefikia malengo aliyoyaweka katika kipindi atakacho kua madarakani ''alisema Mike Pompeo.

Aidha Trump amesema kuwa mkutano huo utaleta matokeo makubwa kwa dunia.

Lakini wakosoaji wa siasa za marekani wanasema kuwa mazungumzo hayo yakienda vibaya basi nchi hizo mbili zitakua na uhusiano mbovu Zaidi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii