Sababu za Moise Katumbi kuanzisha Chama akiwa Afrika Kusini

Katumbi

Mfanyabiashara maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi ambaye sasa amejitosa kwenye ulingo wa siasa, anazindua chama chake akiwa Afrika Kusini.

Katumbi ni kiongozi wa upinzani ambaye yupo uhamishoni kutoka DR Congo baada ya kutengana na Rais Joseph Kabila.

Katumbi ambaye amewahi kuwa Gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo ,Katanga alijiuzulu na kumshtumu rais Kabila kwa uongozi duni.

Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo na anayetarajiwa kumpa rais Kabila ushindani mkali endapo atawania tena.

Alitangaza kutaka kuwania urais mwaka 2016, kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa.

Katumbi aliondoka DRC Mwezi Mei mwaka 2016 na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu punde tu aliposhutumiwa kuwaajiri wapiganaji. Baada ya hapo alihukumiwa bila yeye kuwepo kwa kuuza maeneo kinyume cha sheria na kupatiwa kifungo cha miaka 3 jela.

Anakanusha tuhuma hizo na amewahi kusema kuwa bado anataka kuwania urais katika uchaguzi utakaofuata. Bw Katumbi pia ni Rais wa klabu ya soka maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya TP Mazembe.

Image caption Bw Katumbi pia ni Rais wa klabu ya soka maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ya TP Mazembe.

Historia ya Katumbi

  • Jina lake la mwisho pia Tshapwe
  • Anajulikana kama Moses Katumbi nchini Zambia, ambapo aliishi kwa miaka mingi
  • Tarehe ya kuzaliwa 28 Disemba 1964
  • Eneo la kuzaliwa ni Kashobwe
  • Ni kabila la Babemba
  • Ni kaka wa kambo wa Katebe Katoto, maarufu kama Rafael Soriano, na mfuasi wa Laurent Nkunda
  • Baba yake ni Padre Nissim Soriano, Mitaliano Myahudi kutoka Rhodes
  • Mama yake ni Virginie Katumbi, kutoka familia ya kifalme ya Kazembe
  • Rais wa kalbu ya Soka TP Mazembe Football iliopo Lubumbashi
  • Anajullikana kwa mapenzi yake na kofia za mtindo 'Cowboy'
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabingwa mara tano wa Afrika TP Mazembe wakishika kombe la Shirikisho