Wapenzi wa jinsia moja wataka kutambuliwa Ghana

Ghana Haki miliki ya picha Philcollins Agbedanu Kröge
Image caption Wapenzi wa jinsia moja nchini Ghana

Jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja nchini Ghana wanataka kura ya maoni ipigwe ili kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja.

Jumuiya hiyo inasema kwamba wanaamini kuna wapenzi wengi wa jinsia moja nchini Ghana ingawa wengi wao huwa wanajificha kwa kuhofia kunyanyaswa na kutengwa na jamii.

Vitendo vya jnsia moja nchini Ghana havikubaliki kisheria,madhehebu mengi pamoja na wanasiasa wanapinga kuruhusiwa kwa vitendo vya jinsia moja kuhalalishwa kisheria.

PhilCollins Agbedanu Kröger ni mwanaharakati aliyemshtumu spika Mike Oquaye kwa kutokuwa na usawa katika kutoa maamuzi dhidi ya haki za wapenzi wa jinsia moja.

"Wapenzi wa jinsia moja sio suala la mtu mmoja hivyo jambo hili linapaswa kujadiliwa katika bunge na kuwataka watu wapige kura ya maoni."

Haki miliki ya picha Philcollins Agbedanu Kröger
Image caption Moja ya vipeperushi vinavyosambazwa kushinikiza kuwa na kura ya maoni kuhusu wapenzi wa jinsia moja nchini Ghana

Msukumo kutoka kwa jumuiya hii ya wapenzi wa jinsia moja imepelekea Balozi wa Marekani nchini Ghana, Robert Jackson amebainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wapenzi wa jinsia moja wakakubalika kisheria nchini Ghana katika karne hii.

Aidha balozi huyo amesema takwimu zinaonyesha kwamba 10% ya watu huzaliwa wakiwa na hisia za kuwa mapenzi ya jinsia moja.

Na anadhani kuna watu wengi zaidi ambao ni wapenzi wa jinsia moja zaidi ya hata Waghana wenyewe wanavyodhani lakini kutokana na jamii kuwatenga hivyo wapenzi hao wa jinsia moja uamua kufanya mahusiano yao kuwa ya siri.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii