Je,vazi la Hijab linaweza kutambuliwa na wanamichezo kimataifa?

Unguja
Image caption Timu ya mpira wa kikapu ya wasichana,Unguja

Hijab ni vazi lenye staha kwa mwanamke wa kiislamu, vazi ambalo linamuwezesha mwanamke huyo kujistiri kikamilifu na kuonyesha heshima aliyonayo katika jamii husika, lakini vile vile kumuenzi mwenyezi Mungu.

Yawezekana hukuwahi kufikiria kuwa Hijab yaweza kutumiwa kama sare ya michezo kutokana na michezo mingi kuwa inachezwa katika mavazi ambayo yanamuacha wazi mchezaji ili aweze kuwa huru katika uchezaji wake.

Kisiwani Zanzibar, hali ni tofauti ambapo vazi la hijab linatumika kama sare maalum ya mchezo wa kikapu.

Image caption Timu ya wasichana ya mpira wa kikapu kisiwani Zanzibar

Sare hii ya hijab ilianzishwa kutokana na ugumu wa wazazi na walezi kuruhusu watoto wao kushiriki katika michezo kwa vigezo vya kuenzi mila na desturi ya eneo husika na kutoenda kinyume na imani yao.

Fatma Said Hammed ni mwanaharakati wa michezo mwenye umri wa miaka 24.

Yeye alipata fursa ya mafunzo kutoka Young Leaders Foundation huko nchini Marekani.

Mafunzo ambayo yamemuhamasisha kuanzisha klabu za timu ya mpira wa kikapu katika shule za sekondari kwa ajili ya wasichana pekee.

Fatma anasema watu wanapenda kukubali kufanya kitu kwa kuona mfano.

Image caption Mwanaharakati wa michezo kwa watoto wa kike

Fatma anaona mbinu hii inafanikiwa kwa kuwa watu wengi wanavutiwa kumuona yeye na kuanza kuamini kuwa hata watoto wao wataweza kuwa kama yeye.

"Pingamizi kubwa lilikuwa ni mavazi, kwa sababu waliona kwenye michezo watu wengi huenda kuwaangalia na kuwashabikia wakati wanaona kuwa wanamichezo wengi huwa hawajajistiri"

Kutokana na pingamizi ambalo watu wengi katika jamii hiyo wanalo ilimfanya kuwa na sare maalum ambayo itakuwa imemsitiri mwili wote wakati wa kucheza.

Sare inayomuhitaji mchezaji avae hijabu, suruali na tisheti yenye mikono mirefu ili mchezaji asionekane sehemu yoyote ya mwili wake.

Kwa upande wa wanafunzi wenyewe ambao wako kwenye timu hiyo wanaona kuwa huo ni mwanzo mzuri kwao na fursa ya wao kuweka kipaumbele katika michezo.

Hajet Haji ni miongoni mwa vijana waliopata ugumu kutoka kwa wazazi wao wakati alipotaka kuingia katika timu hiyo. Lakini sasa anaona mabadiliko.

Lakini pia muda anaotumia katika michezo unamfanya aepuke vishawishi kutoka kwa marafiki.

Image caption Mwanafunzi anayejivunia kuvaa hijab katika michezo

Aidha kwa upande wa dini ambayo imekuwa sababu kuu inayowafanya wazazi wengi katika kisiwa hicho cha Unguja kukataza watoto wao wa kike kushiriki katika michezo.

Umri Kuruthum Ali ambaye mwenye umri wa miaka 17 anasema baada ya kugundua kuwa anaweza kucheza mpira wa kikapu akiwa amevalia hijab sasa anaweza kuogelea vizuri na kucheza mpira wa tenis akiwa amevaa hijab pia.

"Na hapa Zanzibar watu wengi wamehamasika sana…faida kubwa ambayo anaioana ni katika upande wa afya,ni mara chache sana kwake yeye kuugua."

Maalimu Hamed Abdalla ambaye ni mlezi na mwalimu wa dini, anasema suala hili linategemea na jamii husika.

"Jamii zinatofautiana, wapo ambao wanakubali mazoezi na michezo na wapo wanaopinga michezo, na kwa wale wanaokubali wanataka wanawake wawe wanacheza bila kuchanganyika na jinsia nyingine."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii