Pakistan wachukizwa na kipindi cha urembo wa rangi nyeusi katika runinga

ubaguzi wa rangi bado upo Pakistan Haki miliki ya picha JAGO PAKISTAN JAGO/HUM TV
Image caption ubaguzi wa rangi bado upo Pakistan

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Pakistan wamekasirishwa na kipindi maarufu cha runinga nchini humo ,kwa kuonyesha wanamitindo waliokuwa wamepaka vipodozi vya rangi nyeusi.

Licha ya kuwa watumiaji wa rangi hizo za urembo wameonesha kuvutiwa na aina ya upakaji wao katika mitandao,

lakini watu wengi wamekosoa kipindi hicho kinachofananisha wapakistani na watu wenye ngozi nyeusi.

Kipindi hicho kilionyesha washiriki wakiwa wanaelekeza namna ya kutumia vipodozi vya rangi nyeusi katika ngozi zao kama sehemu ya urembo.

Mjadala uliozushwa kwenye mtandao juu ya kipindi hicho kuna walioandika katika mtandao kuwa ubaguzi wa rangi haukubaliki sio kwa mashariki au magharibi, sio popote.

Ni muda mrefu sasa tumejifunza hili.

"Sio sahihi pia kusema matumizi ya urembo wa rangi nyeusi katika uso ni jambo baya,wao pia uvutia katika urembo wao.

Raia wa marekani mwenye asili ya Pakistani Bi.Saher Sohail ambaye anaendesha ukurasa maarufu wa vichekesho instagram ameonekana kutojali hilo.

"Mlikuwa mnawaza nini"? Aliuliza. "Wakati baadhi yenu mkinishirikisha jambo hili, kwa kweli kwa Mungu haiaminiki hivyo,"

Andiko hilo mtandaoni lilipendwa na watu zaidi ya milioni saba.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walimwandikia moja kwa moja katika ukurasa wa Instagram wa mwendeshaji wa kipindi hicho cha runinga na mwigizaji wa kike Sunam Jung

kuuliza kwa nini bado haombi radhi?

Huku wengine wakiandika ujumbe wa matusi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii