Rais pekee wa kike barani Afrika ataachia ngazi

Ameenah Gurib-Fakim ni mwanamke wa kwanza Mauritius kupata urais mwaka 2015 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ameenah Gurib-Fakim ni mwanamke wa kwanza Mauritius kupata urais mwaka 2015

Wakili wa Rais pekee wa kike barani Afrika, rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim amesema rais huyo ataondoka ofisini kwake siku ya ijumaa.

Bi.Gurib-Fakim amekuwa akituhumiwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha.

Licha ya kwamba bi.Gurib-Fakim amekanusha madai hayo ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwenye kadi ya benki ya shirika la msaada kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

Lakini siku moja baada ya kukataa wazo la kujiuzulu wakili wake Yusuf Mohamed aliwaambia waandishi wa habari wa nchi hiyo kuwa rais huyo atajiuzulu.

Mpaka sasa rais mwenyewe hajatoa tamko lolote kuhusu yeye kuachia ngazi.

Waziri mkuu wa nchi hiyo alisema rais huyo angeachia wadhifa wake jumatatu iliyopita, jambo ambalo halikufanikishwa .

Hofu ya mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ulianza baada ya rais huyo kugoma kujiuzulu.