Mkurugenzi wa FBI aliyefutwa kazi 'amwaga mtama' kuhusu mazungumzo na Trump

Close-in shot of Andrew McCabe testifying before a House Appropriations subcommittee in June 2017 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mr McCabe was fired on Friday, two days short of his expected retirement date

Naibu mkurugenzi wa zamani katika shirika la ujasusi nchini Marekani FBI Andrew McCabe ametoa barua kuhusu mazungumzo aliyokuwa nayo na rais wa Marekani Donald Trump kwa kamati inayochunguza 'mkono' wa Urusi katika uchaguzi wa urais wa 2016 , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Barua hizo huenda zikasaidia madai kwamba rais Trump alitaka kuzuia haki kufanyika. Bwana McCabe alifutwa kazi katika shirika la FBI siku ya Ijumaa .

Bwana Trump alimtuhumu kwa kufanya upendeleo na kusema siku ya Jumapili kwamba Bwana McCabe hakuandika walichokuwa wakizungumzia.

Rais huyo pia alipuuzilia mbali uchunguzi huo wa Urusi akisema kuwa 'anaandmwa kisiasa'. Uchunguzi huo unaongozwa na wakili maalum Robert Mueller ,ambaye ni mkurugenzi wa zamani wa FBI .

Kufikia sasa amewashtaki watu 19. Wakili wa rais John Dowd alitoa taarifa siku ya Jumamosi akisema kuwa ni wakati uchunguzi huo wa wakili maalum unafaa kutamatishwa.

Bwana Trump amelalamika kwamba kundi hilo la Mueller linashirikisha wanachama 13 wa chama cha Democrats , wafuasi wa Hillary Clinton na hakuna wananchama wa Republicans.

Kwa nini McCabe alifutwa kazi na Trump?

Bwana McCabe alikuwa akichunguzwa na FBI na alikuwa tayari amejiondoa kwa muda katika wadhfa wake mnamo mwezi Januari akisubiri matokeo ya uchunguzi huo.

Alipigwa kalamu siku mbili kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya 50 siku ya Jumapili alipotarajiwa kustaafu kupitia pensheni ya kijimbo.

Mwanasheria mkuu Jeff Session alisema kuwa uchunguzi ulisema kuwa bwana McCabe alitoa matamshi yasiofaa chini ya kiapo mara kadhaa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa itawacha uamuzi wa kumpiga kalamu bwana McCabe (right) kwa bwana Sessions (left)

Ijapokuwa uamuzi wa kumfuta kazi McCabe ulifanywa na bwana Sessions, Bwana Trump alimkosoa kwa miezi kadhaa.

Amekuwa akizungumzia kuhusu michango ambayo mke wa McCabe alipokea kutoka kwa mwandani wa Clinton , mfuasi wa Democrat wakati alipogombea wadhfa wa seneti 2015 na kwamba bwana McCabe alikuwa akipendelea upande mmoja wa kisiasa.

Mnamo mwezi Disemba Trump alituma ujumbe wa Twitter: "Naibu mkurugenzi wa FBI Andrew McCabe anataka kustaafu na mapato yote aliyofanya kazi .Siku 90 zimesalia!!!!

Alipongeza hatua hiyo ya kufutwa kazi muda mfupi tu baada ya bwana Session kutangaza akisema kuwa ni siku njema kidemokrasia. Hatua ya bwana Trump kutuma ujumbe wa twitter kuhusu hatua hiyo ilizua hisia kali kutoka kwa mkurugenzi a CIA John Brennan ambaye alisema kuwa bwana McCabe alikuwa akitumiwa vibaya.

Je barua hizo zinasema nini?

Habari kwamba bwana McCabe aliweka rekodi ya mazungumzo yake na rais Trump wakati alipokuwa akishikilia wadhfa wa mkurugenzi wa FBI zilizuka siku ya Jumamosi.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinasema kuwa barua hizo zitamsaidia bwana Comey kuhusu sababu zilizopelekea yeye kufutwa kazi mwezi Mei uliopita.

Image caption Mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey

Bwana Comey alitoa ushahidi kwamba bwana Trump alimtaka kuwa mtiifu na mwaminifu huku akimuomba kufutilia mbali uchunguzi wa aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn.

Yeye pia anasema kwamba alihifadhi mazungumzo yake na rais Trump.

Lakini rais Trump alipuuzilia mbali rekodi hizo za mazungumzo yao , akichapisha ujumbe wa Twitter siku ya Jumapili akisema kwamba alikuwa na muda mfupi sana na bwana McCabe -kaimu huyo mkurugenzi na kwamba hakuandika chochote wakati wa mkutano wao asubuhi.

''Sawa na muongo James Comey .Je tunaweza kuziita barua za uongo?'', aliuliza rais Trump

Akijibu hatua yake ya kupigwa kalamu, bwana McCabe alikana kufanya makosa yoyote. ''Nimefutwa kazi kutokana na jukumu nililochukua na matokeo baada ya kufutwa kazi kwa James Comey'' , alisema.

Taarifa hiyo inadai kwamba idara ya haki ilipendekeza kufutwa kwake baada ya kudai kwamba ataunga mkono visa vilivyomkumba James Comey.

Siku ya Jumamosi bwana Comey ambaye anatarajiwa kuchapisha kitabu alisema kuwa raia wa Marekani hivi karibuni wataweza kujionea wenyewe nani mheshimiwa baada ya rais huyo kumshutumu tena siku ya Jumamosi.

Rais Trump alisema nini siku ya Jumamosi?

Rais Trump aliendelea kuchapisha ujumbe katika Twitter kuhusu kuondoka kwa bwana McCabe katika mitandao ya kijamii akisema kuwa kumekuwa kukivuja, uwongo na ufisadi katika shirika la kijasusi la FBI pamoja na idara ya ulinzi na wizara ya mawala ya kigeni.

Katika barua pepe, mtandao wa Daily Beast ulisema kuwa wakili wa Trump bwana Dowd aliomba iwapo mwanasheria mkuu Rod Rosenstin atafuata mfano mzuri wa bwana Session kufutilia mbali uchunguzi unaoendelea.

Alisema kuwa taarifa hiyo ilikuwa kwa niaba ya rais kabla ya kukana na kusema kuwa taarifa hiyo ni ya kibinafsi.

Taarifa hiyo ya Dowd ilizua hisia kali kutoka kwa wanachama wa chama cha Democrats wakitaka uchunguzi wa Mueller kutopendelea upande wowote.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii