Watu wawili wajeruhiwa baada ya mlipuko wa vifurushi

Maafisa wa polisi wamelizingira eneo la mkasa wa mlipuko huo. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wa polisi wamelizingira eneo la mkasa wa mlipuko huo.

Mlipuko umewajeruhi watu wawili katika jiji la Austin, kwenye jimbo la Texas baada ya msururu wa mashambulio ya mabomu kwenye jiji hilo.

Vifurushi vitatu vilivyoachwa milangoni vimewaua watu wawili na kuwajeruhi wawili tangu mapema mweza wa Machi.

Polisi hawajathibitisha iwapo shambulio la Jumapili linahusiana na mashambulio hayo mengine lakini wamewaambia wakazi wa eneo hilo wabaki ndani hadi usalama urejee.

Mlipuko wa hivi karibuni umetokea saa kadhaa baada ya tangazo la zawadi ya dola za Kimarekani 100,000 kwa habari zozote zitakazowasaidia polisi.

Zawadi hio ya fedha ni ongezeko kutoka dola za Kimarekani 15,000 zilizotajwa awali na gavena wa jimbo hilo.

Watu wawili waliouawa mapema mwezi huu walikuwa Wamarekani weusi na polisi wanasema chanzo cha sababu za mashambulio huenda ni ubaguzi wa rangi.

Haki miliki ya picha FBI
Image caption Kipeperushi chenye picha wahanga waliouwawa na mashumbilo hayo ikishashawishi watu kutoa habari walionazo kuhusu tukio hilo

Mkuu wa polisi wa Austin, Brian Manley amewaambia waandishi wa habari kuwa anaamini mashambulio hayo yana maudhui ya "kutuma ujumbe flani" .

Bw Manley pia ametoa onyo kwa umma kutogusa vifurushi vyovyote ambavyo hawakutegemea kuvipata.

Mada zinazohusiana