Nani hudhibiti kemikali hatari zaidi duniani?

Wataalam wa kimataifa wakiwa kwenye mavazi maalum ya kuzuia kemikali Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wataalam wa kimataifa wakiwa kwenye mavazi maalum ya kuzuia kemikali

Wataalamu wa kimataifa wanatarajiwa kuwasili Uingereza karibuni kufanya uchunguzi kuhusu sumu ambayo inadaiwa kutumiwa katika jaribio la kumuua jasusi wa zamani kutoka Urusi na binti yake.

Wataalamu hawa hufuatilia vipi sumu hatari duniani na huzidhibiti hivi?

Baada ya kupokea sampuli za sumu iliyotumiwa kumshambulia Sergei Skripal na binti yake Yulia, kundi la wataalamu kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Silaha za Kemikali (OPCW) watafanya uchunguzi wao.

Matokeo yanatarajiwa kutolewa katika kipindi cha wiki mbili hivi.

Serikali ya Uingereza imesema kemikali za sumu zilitumika na Urusi na kukana madai ya Urusi kuwa sumu hiyo ilitoka kwenye vinu vya Porton Down vya Uingereza

Kazi ya OPCW inafanyika ikiwa ni sehemu ya udhibiti unaofanywa kutazama kwa ukaribu kuhusu kipi kinaruhisiwa au hakiruhusiwi linapokuja suala la kemikali zenye sumu.

Mkataba wa mwaka 1997 kuhusu silaha za kemikali CWC, ambao uliwekwa saini na nchi 192, Korea Kaskazini, Israel na Misri hazikutia saini lakini bado vifungu vya sheria vinawafunga.

Nchi zilikubaliana kutotengeneza, kuhifadhi au kutumia silaha za kemikali au kuwasaidia wengine kufanya hivyo.Walitakiwa pia kuweka wazi ni silaha gani za kemikali wanazo au wanataka kuzitengeneza

Maazimio haya hutumiwa na OPCW kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kusimamia uteketezaji wa silaha za kemikali ,mchakato unaotakiwa kutekelezwa ndani ya miaka 10

Nchi nyingi hutekeleza hilo ndani ya muda uliowekwa, isipokuwa Urusi kwa sababu ya ukubwa wa silaha zao, na changamoto ya kuziondoa pia gharama zimesababisha kuchelewesha utekelezaji wake.

Miezi kadhaa iliyopita, Urusi ilitangaza imemaliza kuteketeza takriban tani 40,000 za kemikali hatari, shehena kubwa duniani, hakukuwa na mzozo katika hili kwa kuwa zoezi zima lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu na wataalam kutoka OPCW.

Marekani iliteketeza takriban asilimia 90 ya kemikali, changamoto waliyoipata ni kuwaeleza raia na kuwahakikishia kuwa zoezi hilo ni salama

Lakini vipi kuhusu kemikali nyingine na hasa zenye sumu?

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Maafisa wakifanyia uchunguzi eneo ambalo Sergei and Yulia Skripal walipatikana

Katika maazimio hayo, nchi zinaruhusiwa kuwa na kemikali za sumu kwa ajili ya matumizi salama, yakiwemo ya viwandani, kilimo, utafiti na dawa.

Kwa silaha zilizo muhimu na zinazotambulika na kemikali ambazo zinatumika kutengenezea, zinaweza kutunzwa lakini kwa kiwango maalum.

Watia saini makubaliano hayo wanaruhusiwa kuwa na jumla ya tani moja na sehemu moja ya kuhifadhia, mara nyingi Maabara ambapo kemikali hizi hutengenezwa.

Ukaguzi wa hifadhi hizi unaofanywa na shirika la OPCW hufanyika mpaka kwa kemikali za kiasi kidogo.

Kwa zile zinazotumika kwa kiasi kikubwa viwandani lakini zenye uwezo wa kutengeneza silaha za kemikali huwa kwenye uangalizi wa karibu.

Rekodi za kiasi kinachotengenezwa, kuuzwa, kutumiwa au kutupwa sharti zitunzwe na serikali na taarifa hizo zifikishwe kwa OPCW kila mwaka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Makao makuu ya OPCW The Hague, Uholanzi

Kila mwaka OPCW hufanya kaguzi 400 kwenye maeneo ya viwanda duniani.

Ingawa kemikali za sumu hazijaelezwa kwa OPCW kuwa zinamilikiwa na nchi yeyote, ilibainika miaka ya 90 kuwa zipo.

Sifa za kemikali hizi zingepaswa kuwekwa kwenye hifadhi ya kumbukumbu, ili ziweze kufahamika katika hatua ya awali ikiwa itabainika sumu isiyojulikana ipo kwenye damu ya binaadamu.

Haijulikani kama maabara za Uingereza zimetekeleza hilo.

Lakini ni muhimu kwa wanasayansi kuzibaini kemikali za sumu zilizomuua jasusi wa Urusi na mwanaye kwa kasi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii