Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook

Watu wanataka kujua kiwango cha habari zinazowahusu zimehifadhiwa na kampuni za teknolojia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wanataka kujua kiwango cha habari zinazowahusu zimehifadhiwa na kampuni za teknolojia

Madai kwamba kampuni ya utafiti ya Cambridge Analytica ilitumia vibaya data ya watu milioni 50 wanaotumia Facebook yamefungua mjadala kuhusu ni vipi habari zilizopo katika mtandao huo wa kijamii husambazwa na kwa nani.

Data ni kama mafuta katika mtandao wa facebook, ndio kivutio kikuu cha matangazo ya biashara kwa mtandao huo ambao hujipatia faida kubwa.

Hakuna shaka kwamba facebook ina uwezo wa kujenga habari kuhusu wateja wake kwa mfano wanachopenda, wasichopenda maisha yao na mirengo yao ya kisiasa.

Swali kuu ni nini wanachosambaza kwa watu wengine na ni nini ambacho watumiaji wanaweza kufanya ili kudhibiti habari zao?.

Unataka kujua unachopenda kama nyota wa Hollywood? bonyeza hapa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Cambridge Analytica Alexander Nix aliwaabia wabunge walitumia data kutoka 'tafiti za Facebook'

Tumeona mitihani inayotaka kupima fikra, kufichua wewe ni nani ama hata kuonyesha ni nini ungependa iwapo wewe ni muigizaji anayependeza.

Ulikuwa ujumbe kutoka kwa mtihani mmoja wa facebook - Huu ndio ujumbe wa kidijitali uliodaiwa kutumiwa kuvuna habari za mamilioni ya watu. Mitihani kama hiyo hufanyika kwa hakikisho kuwa data yako iko salama.

Michezo hii na mitihani inalenga kuwavutia wateja wa facebook na inakubalika na masharti ya mtandao huo.

facebook imebadilisha masharti yake kupunguza habari ambazo kampuni nyengine inaweza kuchukua hususan kuwazuia kuchukua habari kuhusu marafiki wa wateja wake.

Bado haijajulikani ni habari gani zilizochukuliwa -hilo ni swala linalochunguzwa na mamlaka ya ulinzi wa data nchini Uingreza ICO.

Nini ambacho wateja wa facebook wanaweza kufanya ili kulinda data yao?

  • Ingia katika facebook na kutembelea Programu iliopo katika ukurasa wa setting
  • Bonyeza kitufe cha edit chini ya programu, tovuti na Plugins
  • Haribu programu iliopo

Hii inamaanisha kwamba hautaweza kutumia watumiaji wa facebook ambao sio marafiki zako na iwapo hiyo ni hatua kubwa kuna njia ya kuzuia kiwango cha habari zitakazotumiwa na programu wakati unapozitumia.

  • Ingia katika ukurasa wa programu ya setting
  • Bonyeza kila orodha ambayo huitaki programu yako kuona ikiwemo bio, siku ya kuzaliwa, familia, dini, iwapo uko katika mtandao , machapisho katika ratiba yako ya data, vitendo na maslahi yako.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alama za vidole zinatumika sana huku watu wakiendelea kusambaziana habari katika mitandao.

"Usibonyeze kitufe cha 'like' katika ukurasa wa bidhaa na iwapo unataka kucheza michezo ama mitahani usiingie kupitia facebook badala yake ingia moja kwa moja katika tovuti hiyo , amesema Paul Bernal muhadhiri wa habari na teknolojia katika chuo cha kusomea sheria cha East Anglia School.

''Ni rahisi kupitia akaunti yako ya facebook , lakini kufanya hivyo kunampatia uwezo mwenye programu hiyo kuona habari nyingi katika ratiba yako ya data'' , aliongezea.

Ni njia ipi nyengine inayoweza kulinda data yako katika facebook?

Kuna njia moja pekee inayoweza kukuhakikisha kuwa data yako haionekani na mtu mwengine kulingana na Bernal. 'Ondoka Facebook'.

''Facebook itaweza kuwalinda zaidi wateja wake iwapo wataanza kuondoka katika mtandao huo. Kwa sasa kuna uwezekano mchache kufanya mabadiliko hayo'', aliambia BBC.

Inaonekana hayupo pekee katika wito huo wa kutoka Facebook.Ujumbe wenye alama ya reli #DeleteFacebook umesambazwa sana katika mtandao wa Twitter kufuatia kashfa hiyo ya Cambridge Analytica .

Lakini Bernal anajua kwamba ni watu wachache watakaotoka katika mtandao huo hususan wale wanaoona facebook kuwa muundo msingi wa maisha yao.

Je unaweza kubaini ni habari gani zinazokuhusu zimehifadhiwa?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mr Schrems amehusishwa katika msururu wa malalamishi dhidi ya facebook tanhgu 2011

Chini ya sheria za kulinda data , watumiaji wanaweza kuwasilisha ombi kwa kampuni binafsi kuhusu kiwango cha data zinazokuhusu ambazo zimehifadhiwa .

Wakati raia wa Austria Schrems aliwasilisha ombi kwa Facebook 2011 , alipewa habari yenye faili 1200 ndani yake.

Alibaini kwamba mtandao huo uliweka rekodi za anwani zote za kampyuta, historia za ujumbe, eneo, mbali na habari alizodhani kuzifuta.

Lakini katika ulimwengu ambapo habari za facebook husambazwa mbali hadi kwa marafiki wa rafikizo , kuwasilisha ombi kama hilo ni vigumu. Kama bwana Bernal anavyosema , unaweza vipi kupata data iwapo hujui ni nani wa kumuuliza?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je unaweza kuonda profile yako katika mitandao yako ya kijamii?