'Kuhamasisha maandamano kupitia mtandao ni kosa la jinai Tanzania'
Huwezi kusikiliza tena

Polisi: Kuhamasisha maandamano kupitia mtandao ni kosa la jinai Tanzania

Polisi mjini Dodoma wanawashikilia watu wawili kwa kosa la kuhamasisha maandamano kwa njia ya mitandao. Mamlaka nchini Tanzania zimekuwa zikidai kwamba maandamano hayo yanalenga kuvunja amani ya nchi.

Polisi imewataja watu hao kuwa dereva na mkulima, ambao wamewashutumu kwa kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano yanayopangwa kufanyika tarehe 26 April mwaka huu

Maandamano hayo kwanza yalipangwa kupitia mitandao ya kijamii na mwanaharakati wa kisiasa aitwaye Mange Kimambi aishiye Marekani.

Bi Kimambi amekuwa akiwahamasisha watu kuandaman kupinga kile anachokiita kuwa ni kuongezeka kwa utawala wa mabavu wa serikali iliyopo madarakani.

Mwandishi wetu Sammy Awami amefanya mahojiano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto na kwanza alianza kwa kumuuliza undani wa kukamatwa kwa vijana hao.