DRC yagomea kongamano la wafadhili Geneva

Umoja wa mataiafa umesema zaidi ya watu milioni 13 wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo wanahitaji misaada ya kijamii. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Umoja wa mataiafa umesema zaidi ya watu milioni 13 wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo wanahitaji misaada ya kijamii.

Serikari ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo imekataa kuhudhuria kongamano na wafadhili, lililopangwa kufanyika mjini Geneva nchini Uswis mwezi ujao kwa madai ya kuwa nchi yao imetangazwa kwa mabaya ulimwenguni.

Umoja wa mataifa umesema kongamano hilo limeandaliwa kwa ajili ya kuchangisha fedha takribani dola bilioni 1.7 za kusaidia binadamu wenye mahitaji nchini DRC.

Anayekaimu nafasi ya waziri mkuu wa DRC, Jose Makila amesema wamekubali kuwa nchi yao ipo kwenye hali ya hatari na yenye kuhitaji msaada lakini amelaumu umoja wa mataifa kwa kuwakatisha tamaa washiriki.

Umoja wa mataiafa umesema zaidi ya watu milioni 13 wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo wanahitaji misaada ya kijamii.

Watu milioni 4.5 hawana makazi maalumu huku wengi wakikumbana na majanga ya vurugu ya kivita.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebarikiwa kuwa na madini mengi pamoja na maliasili lakini zimeathiriwa na vita vinavyosababishwa na vikundi vya waasi ,rushwa na machafuko ya kisiasa.

Umoja wa mataifa imesema hali ya sasa nchini DRC ni ya kusikitisha sana ndio maana wameamua kuandaa kongamano maalumu mjini Geneva kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazowasaidia raia wa Kongo.

Pamoja na hayo waziri Makila amesema Umoja wa mataifa umekuwa ukitoa taswira mbaya wa wahusika na washiriki wa kongamano hilo, hivyo serikali yake imeamua kukataa kushiriki kongamano hilo.

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya kongo Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 huku muhula wake wa pili ukiwa tayari umemalizika tangu desemba mwaka 2016.

Uchaguzi mkuu wa DRC umepangwa kufanyika desemba mwaka huu lakini wengi wanatilia shaka kama Rais Kabila atakubali kuachia madaraka.