Thamani ya facebook yashuka kwa $58bn kufuatia kashfa

Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanzilishi wa Mark Zuckerberg- hisa za Facebook zilianguka kufuatia habari mabaya ya data

Mtandao huo wa kijamii ulikabiliwa na hisia kali kutoka kwa wanasiasa , wawekezaji na wateja wake kufuatia kashfa ya data

Mimiliki wake Mark Zuckerbag aliomba msamaha kufuatia ukiukaji wa sheria ya data ulioathiri zaidi ya watu milioni 50.

Msamaha huo hatahivyi haukuwazuia wawekezaji kutouza hisa zao huku wengi wakishangazwa ni kiwango gani uharibifu huo utaathiri mtandao huo wa kijamii.

Matangazo mabaya dhidi ya facebook yaliwafanya watangazaji wengine wa matangazo kusema 'imetosha Imetosha'.

Hisa katika mtandao huo wa kijamii zilianguka kutoka $176.80 siku ya Jumatatu hadi $159.30 siku ya Ijumaa jioni.

Je hisa hizo zitajinusuru na kuimarika?

Hisa za facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na hivyobasi kuipatia kampuni hiyo thamani ya kibiashara ya $104b.

Kufuatia ukuwaji thabiti na utawala katika matangazo ya kidijitali hisa za facebook zilipanda hadi $190 kufikia Februari mwaka huu.

Brian Wieser mchanganuzi mkuu katika kampuni ya utafiti ya Pivital alisema kuwa alipata matokeo mabaya ya hisa za facebook .

''Nilikuwa nikilenga $152 katika facebook mwaka 2018 na hiyo ilikuwa kabla ya kisa cha kashfa iliotokea wiki hii''.

Bwana Wieser anasema kuwa kushuka kwa bei ya hisa kulionyesha kuwa wawekezaji waliogopa kuongezeka kwa udhibiti mbali na wateja kuondoka katika mtandao huo lakini kulikuwa na hatari chache kwa wamiliki wa matangazo kuondoka facebook.

Watakwenda wapi?, Hargreaves Lansdown , mchanganuzi mkuu Laith Khalaf alisema kwamba wiki iliopita ilikuwa mbaya zaidi katika historia ya facebook.

Mojawapo ya siri na ufanisi wa Facebook , kiwango cha wateja wanaojiunga na facebook kinazidi kuwapendeza wateja wake. La kushangaza ni kwamba ni wembe huohuo unaoinyoa facebook wakati inapopoteza idadi kuu ya watumiaji wake kutokana kashfa hiyo.

Je wito wa wamiliki wa matangazo ni upi?

Mkurugenzi wa kampuni ya matangazo ya M&C Saatchi David Kershaw amesema kuwa ufichuzi kwamba mtihani wa facebook wa 2014 ulivuna data ya watumiaji wa mtandao huo na marafiki zao bila ya idhini umesababisha hisia kali kutoka kwa warushaji matangazo.

Kampuni ya matangazo ya Mozilla na Commerzbank siku ya Jumatano ilisitisha kwa muda matangazo yake katika mtandao huo wa facebook.

Siku ya Jumatano kampuni ya kiteknolojia Elon Musk ilifutilia mbali kurasa za kampuni zake za Telsa and Spaces.

''Usifanye makosa , facebook ni mtandao mzuri sana wa matangazo kutokana na lengo lake likiwa linatoka kutoka data. Lakini nadhani kampuni hizo kubwa zina waiswasi kuhusishwa na chombo ambacho data hutumia vibaya hususan katika kinyang'anyicho cha kisiasa'', alisema Mr Kershaw said.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Facebook imekosolewa kufutaia hatua yake ya kusambaza data ya wateja wake.

Bwana Kershaw aliambia BBC kwamba mabadiliko yoyote katika facebook katika ulinzi wa data yatasababishwa na tishio la wawekezaji wa matangazo kuondoa fedha zao badala ya watumiaji wa mtandao wanaotumia alama ya reli #Deletefacebook na #Boycottfacebook na #Boycottfacebook ambazo zimekuwa na umaarufu.

Kampuni ya matangazo ya UK ISBA ilikutana na Facebook siku ya Ijumaa na ksema kuwa jopo la facebook lililirai kundi hilo kwamba kampuni hiyo ya mtandao ilikuwa inachukua hatua za haraka kuangazia malalamishi ya wamiliki wa matangazo, ikiwemo kukagua programu mbali na mkutano wa ana kwa ana na kampuni zinazoweka matangazo yao katika mtandao huo nchini Uingereza.

Je Zuckerbag ametoa hakikisho kwa wateja wa Facebook?

Mwanzilishi huyo wa facebook alijaribu kuwahakikishia watumiaji wake , hatua muhimu ya kuzuia hilo kufanyika tena ilichukuliwa miaka kadhaa iliopita.

Hatahivyo mwekezaji wa kampuni ya kiteknolojia Passion Capital Eileen Burbidge ambaye pia yuko katika kundi la washauri la waziri mkuu alisema kuwa facebook ilichukua muda mrefu kuwahakikishia watuamiaji wake na wateja wake.

''Swala kwamba mtandao huo ulichukua siku tano kutoa taarifa ambayo ilionekana kuwa na usawa ulikuwa muda mrefu'' , bi Burbidge alisema. ''Nadhani walinyamaza kwa siku nyingi sana''.

Kampuni hiyo imesema kuwa Facebook ilidharau uharibifu uliofanywa na wateja wake walipogundua kwamba baada ya data yake kutumika kisiasa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Data ya watumiaji wa Facebook ilitumika kisiasa katika uchaguzi wa marekani wa 2016

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii