Tetesi za soka Ulaya Jumapili 25.03.2018

Kiungo wa kati wa Man United na Ufaransa Paul Pogba
Image caption Kiungo wa kati wa Man United na Ufaransa Paul Pogba

Manchester United iko tayari kumuuza kiungo wa Ufaransa ,25 Paul Pogba . Wachezaji inaowanyatia ni beki wa Real Madrid Raphael Varane, 24, na kiungo wa kati wa Ujerumani Toni Kroos, 28, beki wa Paris St-Germain na Brazil Marquinhos, 23, na kiungo wa kati wa Itali Marco Verratti, 25, pamoja na beki wa Juventus, 27, raia wa Brazil Alex Sandro. (Sunday Mirror)

Pogba na mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho hawazungumziani baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuwachwa nje na klabu yake mwezi uliopita (Sun on Sunday)

Mourinho hadhani kwamba ''uwezo wa wachezaji'' unaweza kumfuta kazi katika klabu ya Old Trafford. (Mail on Sunday)

Image caption Antonio Conte

Paris St-Germain wamefungua mazungumzo na wawakilishi wa Antonio Conte kuhusu raia huyo wa Itali Kuhamia katika mji mkuu wa Ufaransa kutoka Chelsea mwisho wa msimu huu. (Guardian)

Mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 25, yuko tayari kuipuuzilia mbali Real Madrid na yuko tayari kupewa mshahara wa £200,000 kwa wiki Anfield. (Sunday Mirror)

Image caption Mohamed Salah

Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel amekataa kazi ya kuifunza Bayern Munich kwa sababu yuko katika mazungumzo na Arsenal. (Bild - in German)

Arsenal na Chelsea wanatarajiwa kushindana katika jaribio la kumsajili kipa wa Atletico Madrid na raia wa Slovenia Jan Oblak, 25. (Sunday Express)

Image caption Hector Bellerin

Ajenti wa Hector Bellerin anasema kuwa beki huyo wa Uhispania anafurahia kusalia Arsenal na kwamba hakuna ombi lolote lililowasilishwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (CRC via Sky Sports)

West Ham iko katika harakati ya kumsajili aliyekuwa mkufunzi wa Manchester City Manuel Pellegrini kuwa mkufunzi wake msimu ujao. (Sun on Sunday)

Image caption Kocha wa zamani wa Man City Manuel Pelegrini

Beki wa Albania Elseid Hysaj ameambia Napoli kwamba kuna klabu ambayo iko tayari kutoa dau la Yuro 50m (£43.7m) kama fedha za kumnunua katika kandarasi yake. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ananyatiwa na Arsenal pamoja na Manchester United. (Tuttosport via Talksport)

Manchester United inasema kwamba sababu ya mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez kupigwa picha akila pekee katika uwanja wa mazoezi ni kwamba alisalia nyuma ili kufanya mazoezi ya kupiga mikwaju. (Star on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexis Sanchez

Kiungo wa Manchester City David Silva ameruhusiwa kuondoka katika kikosi cha Uhispania kwa sababu za kibinafsi.. (Independent)

Winga wa Manchester City Leroy Sane amedaiwa kuwa mchezaji mwenye kasi zaidi katiika ligi ya Uingereza msimu huu na pia mwenye kasi zaidi tangu rekodi hiyo ianze kuwekwa 2013-14. (Mail on Sunday)

Image caption Leroy Sane

Mshambuliaji wa Uingereza Jamie Vardy, 31, alikosa kugusa mpira baada ya kuingizwa katika dakika za lala salama dhidi ya Uholanzi lakini anatumai kuanza dhidi ya Itali Jumanne Ijayo. (Guardian)

Takriban mchezaji mmoja wa Uingereza anafikiria ya kuajiri maafisa wake wa usalama ili kusafiri na familia yake katika kombe la dunia la mwisho wa msimu huu huko Urusi.. (Telegraph)

Beki wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen anasema kuwa wanalenga kufika nusu fainali ya kombe la dunia katika kundi ambalo linaorodheshwa Uingereza . (Telegraph)

Mada zinazohusiana