Watu 64 wafariki katika mkasa wa moto jumba la Kemerovo, Urusi

Firefighters extinguish a fire at a shopping mall in Kemerovo, Russia March 25, 2018 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dari la jumba moja kubwa la kibiashara linadaiwa kuporomoka

Watu 64 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la kibiashara katika mji maarufu kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi.

Watu zaidi ya 64 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto 41.

Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka.

Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry.

Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema.

Video zilizopakiwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka nje kupitia madirisha kujaribu kujinusuru kutoka kwa moto huo uliozuka Jumapili.

Wazima moto zaidi ya 660 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji.

Chanzo cha moto huo hakijabainika lakini maafisa wameanzisha uchunguzi.

Kemerovo, ni eneo maarufu sana kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe.

Ni mji unaopatikana takriban kilomita 3,600 mashariki mwa mji mkuu Moscow.

Kansela wa Austria Sebastian Kurz ametuma salamu zake za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waathiriwa, sawa na Waziri wa mambo ya nje wa Latvia Edgars Rinkēvičs.

Moto ulianza vipi?

Kando na kumbi nyingi za sinema, jumba hilo, ambalo lilifunguliwa mwaka 2013, lina migahawa kadha, na vituo kadha vya bafu za maji ya mvuko, kito cha mchezo wa bowl na kituo cha kujumuika na wanyama.

Moto unaaminika kuanza mwendo wa saa 17:00 (10:00 GMT) kwenye sehemu ya jengo hilo ambayo ina kumbi za burudani, vyombo vya habari Urusi vinasema.

"Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba dari liliporomoka katika kumbi mbili za sinema," Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imesema kupitia taarifa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moto ukifuka kutoka kwa jengo hilo

Yevgeny Dedyukhin, naibu mkuu wa idara ya huduma za dharura katika eneo la Kemerov, wamesema eneo ambalo liliathiriwa na moto huo ni la ukubwa wa mita 1,500 mraba.

"Jumba hili limejengwa kwa njia ambayo inatatiza juhudi za kudhibiti moto," alisema.

"Kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kushika moto."

Haki miliki ya picha Alexander Korovin
Image caption Moto huo ulianza katika eneo lililo na chumba cha burudani na ukumbi wa sinema

Tunafahamu nini kuhusu waathiriwa?

Miili ya watu 37 ambayo ilikuwa imeungua kiasi cha kutotambulika imegunduliwa, kwa mujibu wa Bw Dedyukhin.

Lakini tisa kati ya waliofariki ni watoto.

Andrei Mamchenkov, naibu mkuu wa Kituo cha Kudhibiti Mikasa cha Taifa Urusi, amesema shughuli ya kuwatafuta watoto 41 inaendelea.

Maafisa wa kuzima moto wameshindwa kufikia moja ya kumbi za sinema zilizokuwa kwenye ghorofa ya tatu juu ya moshi na hatari ya jengo kuporomoka, afisa mmoja ambaye hakutana jina lake litajwe amenukuliwa na shirika la habari la Urusi la Interfax.

Mdokezi mwingine ameambia shirika hilo kwamba kwa sasa hawatarajii kupata manusura.

Mada zinazohusiana