Miguna Miguna akataliwa kuingia Kenya

Bw Miguna Miguna (kwanza kushoto) wakati Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo kuwa Rais wa Wananchi Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Bw Miguna Miguna (kwanza kushoto) wakati Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo kuwa Rais wa Wananchi

Mwanansheria wa upande wa upinzani wa Kenya,Miguna Miguna amekataliwa kuingia Kenya baada ya kukataa kuomba Visa, gazeti binafsi la The Star la ripoti.

Bwana Miguna anasafiri kwa kutumia kibali chake cha kusafiria cha Canada baada ya kuvuliwa uraia wa Kenya.

Image caption Mfuasi wa upinzani alikuwa akimsubiri wakili Miguna Miguna katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta

Mamlaka ya Kenya ilimrudisha Canada baada ya kushiriki katika kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama "Rais wa watu".

Wiki iliyopita Miguna aliiambia BBC kuwa mamlaka ya Kenya haijafuata maagizo ya mahakama ya kumpatia hati za kusafiria za Kenya.

Serikali ya Kenya ilimvua uraia Miguna na kumrudisha Canada ambapo pia ni raia huko.

Mahakama ya kenya ilitoa amri kwa serikali hiyo kurudisha hati za kusafiria za Miguna na kusaidia katika kurejea kwake lakini kwa mujibu wa Miguna serikali haija fanya hivyo.

Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi ambaye alikwenda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta amesema vyanzo vinasema serikali inataka kumpa visa ya muda wa miezi sita na kuchukua pasipoti yake.

Image caption Hamu na Ghamu: Jinsi waandishi walivyongang'ania kumsubiri Miguna katika mlango wa Mapokezi

Waandishi wa habari wa Kenya wamekusanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta uliopo Nairobi, ili kupata taarifa ya ujio wa wakili huyo wa upinzani Miguna Miguna ambaye aliondolewa Kenya tangu tarehe 6 mwezi Februari mwaka huu.

Mada zinazohusiana