Mahakama Kenya yaagiza Miguna aachiliwe

Bw Odinga alijaribu kumsaidia Bw Miguna kuondoka uwanja wa ndege bila mafanikio Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Awali Bw Odinga alijaribu kumsaidia Bw Miguna kuondoka uwanja wa ndege bila mafanikio

Jaji wa mahakama kuu Roseline Aburili ameagiza wakili wa upande wa upinzani Miguna Miguna kuachiliwa kutoka kwa uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta.

Miguna ameagizwa kutokea mahakamani kesho Jumatano sasa tatu saa za Afrika Mashariki.

Image caption Maamuzi ya mahakama

Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

Miguna Miguna: Wakili aliyeidhinisha kiapo cha Odinga azuiliwa uwanja wa ndege Nairobi

Haki miliki ya picha Waikwa Wanyoike
Image caption Hali ilivyokuwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta siku ya Jumanna, Miguna alikesha kwenye uwanja huo.

Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

Mada zinazohusiana