Mwanamume apatwa na 'kisonono kibaya duniani'

Mwanamume aliyepatikana na ugonjwa wa kisonono Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanamume aliyepatikana na ugonjwa wa kisonono

Mwanamume mmoja nchini Uingereza amesemekana kuwa na kesi "mbaya zaidi" duniani ya ugonjwa wa Kisonono.

Alikuwa na mpenzi mmoja nchini Uingereza lakini alipata bakteria hiyo baada ya kujamiana na mwanamke mmoja kutoka Kusini Mashariki mwa Asia.

Madaktari wa afya huko Uingereza wamesema kwa mara ya kwanza kwamba maambukizi hayo hayawezi kutibika na dawa aina za 'antibiotics'

Maafisa hao sasa wanamtafuta mpenzi yeyote wa mwanamume huyo, ambaye bado hajulikani, kama njia ya kujaribu kuzuia usambazaji zaidi.

Mwanamume huyo alipatwa na mambukizi hayo mapema mwaka 2018.

Tiba halisi ya ugonjwa huo ni mchanganyiko wa dawa aina ya azithromycin na ceftriaxone lakini zimeshindwa kuutibu ugonjwa huo.

Dkt Gwenda Hughes, wa kituo cha afya cha Uingereza amesema: ''Hii ni mara ya kwanza kwa kesi kama hiyo kudhihirisha kiwango kikubwa cha kutosikia kwa dawa hizo mbili zinazotumika sana za antibiotics.

Majadiliano na Shirika la Afya Duniani(WHO) na kituo cha ulaya kinachodhibiti magonjwa wamekubaliana kwamba kisa hicho ndicho cha kwanza kutokea duniani.

Kisonono ni ugonjwa gani?

Haki miliki ya picha CAVALLINI JAMES/SCIENCE PHOTO LIBRARY
Image caption Bakteria ya kisonono

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria kwa jina Neisseria gonorrhoeae.

Maambukizi hayo husambazwa na ukosefu wa kinga mtu anapofanya kitengo cha ngono.

Kwa wale walioambukizwa, mwanamume mmoja kati ya10 na zaidi ya robo tatu ya wanawake na mashoga dalili za ugonjwa huo hazibainiki kwa haraka.

Dalili za ugonjwa huo zinajumuisha;

  • Ute mzito wa rangi ya jani au manjano kutoka katika sehemu za siri,
  • Uchungu unapokojoa
  • Uvujaji damu wakati mwengine.

Maambukizi hayo wasipotibiwa yanaweza kusababisha mtu kukosa mtoto, kufura katika sehemu za siri na unaweza kusambazwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto aliyetumboni.

Utafiti wa mwanamume huyo unabaini kwamba 'antibiotic' ya mwisho inaweza kufanya kazi . Kwa hivi sasa anapokea matibabu na madaktari watapata matokea baada ya mwezi mmoja iwapo watafaulu.

Kwa hivi sasa hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa -hata mpenzi wake wa Uingereza amegunduliwa lakini uchunguzi bado unaendelea.

Dkt Hudhes aliongeza: ''Tunafuatilia kesi hii ili kuhakikisha kwamba maambukizi hayo yametibiwa vilivyo na mapendekezo mengine na hatari za maambukizi kwa siku zijazo kupunguzwaa.''

Dkt Olwen Williams, rais wa muungano wa Uingereza wa maswala ya afya ya ngono na virusi vya HIV: ''Kutokea kwa maambukizi hao ambayo hayasikii dawa ya kisonono ni jambo la kuzingatiwa na maendeleo makubwa.

''Tunawasiwasi kwamba shida hii inaweza kuongezeka kutokana na upungufu uliofanyiwa bajeti ya afya.

''La kusikitisha kabisa ni kwamba kesi hii imeiwacha huduma ya afya ya ngono katika nafasi ''mbaya'' huku kliniki zikifungwa katika wakati mgumu zaidi.