Watu wafupi waunda klabu yao ya soka Kenya

Watu wafupi waunda klabu yao ya soka Kenya

Watu walio na kimo kifupi, kwa jina la kitaalam vibete, wanapitia changamoto mbalimbali.

Wakiwa na kimo kisichozidi futi 4 inchi 10, wengi hukumbana na ubaguzi na unyanyapaa katika jamii.

Hata hivyo, shirika moja nchini Kenya, linalojumuisha watu walio na kimo kifupi limebuni klabu ya soka, ya kwanza kabisa nchini humo, yenye lengo la kukabiliana na unyanyapaa ndani ya taifa hilo na pia kimataifa.

Anthony Irungu aliitembelea klabu hiyo.