Afrika Wiki hii katika picha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku ya Jumanne ,siku ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Misri ,mwanamama akicheza mbele ya Bendera jijini Cairo
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bado kuna shamrashamra siku ya pili.Yanaonekana mabango yanaohamasisha raia kupiga kura
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kulikuwa na ulinzi mkali wakati wa kupiga kura, wapinzani wakuu walitolewa au kuzuia kugombea
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Upande mwingine wa bara, wtu wanasheherekea nje ya Mahakama kuu baada ya kuamriwa ufanyike uchaguzi wa marudio siku ya Jumamosi nchini Sierra Leone
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wapiga kura wanajiuliza wagombea watafanya nini kuhakikisha uchumi unaimarika, baadhi ya watu,kama mwanamke huyu ni miongoni mwa watu fukara duniani
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Jumanne, wacheza ngoma za utamaduni walikuwa wakitumbuiza katika mkutano wa kumuaga Rais Seretse Ian Khama nchini Botswana
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mama huyu alifika kwenye mkutano huo kutoka kwenye kijiji cha Serowe anachotoka rais Seretse
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku ya Jumatano, Mwanasiasa Hassan Ayariga alionekana akiwa amepanda Farasi jijini Accra, akipinga Ripoti kuwa Jeshi la Marekani litaanza kuweka kambi yake nchini Ghana
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Alhamisi, Kimbunga cha vumbi kilikumba mji wa Khartoum nchini Sudan.Mamlaka zililazimika kuahirisha safari na shule kufungwa
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Ijumaa, Bajaji ilionekana kwenye mabaki baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwenye Gari kulipuka kwenye mtaa wenye pilika nyingi mjini Mogadishu nchini Somalia
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watoto wa shule wakisubiri kumsalimia Rais wa Namibia, Hage Geingob
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Jumatano,mcheza Kriketi wa Australia Steve Smith anaonekana pichani akiondoka nchini Afrika kusini baada ya kubainika kuwa alitumia karatasi ya msasa kuuharibu mpira wakati wa mechi ya tatu kati ya nchi hizo mbili
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Jumapili mchezo wa fainali kuwania Kombe la Rugby nchini Kenya ulipigwa
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wavulana wakicheza mpira wa miguu kusini mwa Jangwa la Sahara nchini Morocco, wakati wa tamasha la kimataifa la jamii ya watu wanaohamahama