Huenda ukurasa wako wa kijamii ukachunguzwa iwapo utaomba Visa ya Marekani

Wanawake wawili walipigwa picha wakiangalia simu zao za mkononi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ikiwa pendekezo la wizara ya mambo ya nje ya Marekani litaidhinishwa linaweza kuwaathiri watu wapatao milioni 14.7 kwa mwaka

Utawala wa Trump umesema kuwa unataka kuanza kukusanya historia ya mitandao ya kijamii ya karibu kila mtu anayetaka visa ya kuingia Marekani.

Pendekezo hilo , ambalo limetolewa na wizara ya mambo ya nje, litawataka wengi miongoni mwa waombaji wa visa kutoa maelezo yao ya akaunti zaoi za Facebook na Twitter

Watatakiwa kufichua majina ya akaunti zao zote za mitandao ya kijamii waliyotumiwa katika kipindi cha miaka mitano ya nyuma

Takriban watu milioni 14.7 wataathiriwa na pendekezo hilo.

Taarifa hizo zitatumiwa kutambua na kuwachunguza watu wanaoomba viza za uhamiaji pamoja na zisizo za uhamiaji.

Waombaji wa visa pia wataulizwa kuhusu nambari za simu walizotumia katika kipindi cha miaka mitano, barua pepena historia yao ya kusafiri.

Watatakiwa kusema ikiwa hawajawahi kurejeshwa kwa lazima kutoka nchi waliyotembelea kwa lazima , ama ikiwa kuna ndugu yao yeyote aliyewahi kuhusika katika harakati za ugaidi .

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Pendekezo hilo litazidisha masaibu kwa wasafiri ambao nchi zao hazina mkataba na marekani wa kuziondolea visa

Pendekezo hili halitawaathiri raia kutoka nchi ambazo Marekani ilizipa hadhi ya kutokuwa na visa - miongoni mwake Uingereza , Canada, France na Ujerumani . Hata hivyo raia kutoka nchi ambazo hazijapewa hadhi hiyo kama India, China na Mexico wanaweza kujipata katika hali ngumu kama wataitembelea Marekani kikazi ama kwa mapumziko.

Chini ya sheria iliyowekwa mwezi Mei mwaka jana, maafisa waliambiwa wachunguze kurasa za mitandao ya kijamii ya watu ikiwa tu wanahisi kufanya hivyo " kwamba taarifa za aina hiyo zinahitajika kuthibitisha utambulisho ama kufanya uchunguzi wa kina zaidi kwa ajili ya usalama wa taifa ", ilisema wizara ya mambo ya nje wakati mmoja.

Pendekezo hilo linakuja baada ya rais Trump kuahidi kutekeleza''uchunguzi mkali'' kwa raia wa kigeni wanaingia Marekani, jambo ambalo alisema lilikuwa ni moja ya mkakati wa kupambana na ugaidi.

"Kuimarisha viwango vya upelelezi mkali kwa waombaji wa visa ni kazi inayotakiwa kufanywa vizuri ili kukabiliana na vitisho vilivyopo," ilieleza taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni, iliyonukuliwa nagazeti la New York Times.

"Tayari tunaomba taarifa chache zamuombaji wa visa kama vile historia ya muombaji, taarifa za wanafamilia, na anuani za awali kutoka kwa waombaji wote wa visa.

Kukusanywa kwa taarifa hizi zote kutoka kwa waombaji wa visa kutaimarisha mchakato wetu wa kuwachunguza wahamiaji hawa na kuthibitisha utambulisho wao ."

Wazo hili litatakiwa kuidhinishwa na ofisi ya Utawala na Tna bajeti ya Marekani.

Umma utakuwa na miezi miwili ya kutoa maoni yake juu ya pendekezo hili kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi rasmi wa utekelezwaji wake.

Hata hivyo makundi yanayochunguza uhuru wa raia yamelaani sera hii wakiitaja kuwa ni uingiliaji wa masuala binafsi jambo linaloweza kuathiri uhuru wa kujieleza.

"Watu sasa wataanza kufikiria juu ya ikiwa kile wanachokisema mtandaoni kitachukuliwa ama kueleweka vibaya na afisa wa serikali ," alisema Hina Shamsi kutoka Muungano unaopigania uhuru wa raia nchini Marekani -( American Civil Liberties Union).

" Pia tuna hofu juu ya namna utawala wa mtizamo wa Trump kuhusu maneno yanayofaa ama yasiyofaa '' kuhusiana an shughuli za ugaidi ' kwasababu neneo ugaidi lilikuwa ni la kisiasa na linaweza kutumiwa kuwabaguwa wahamiaji ambao hawajafanya kosa lolote ," alisema .

Mitandao ya kijamii iliyohusishwa na pendekezo hilo ni pamoja na Instagram, LinkedIn, Reddit na YouTube. Hata hivyo gazeti la New York Times linaripoti kuwa mitandao ya nchi za nje kama vile ule wa Uchina wa Weibo na wa Urusi VK pia itajumuishwa..