Arnold Schwarzenegger yuko ''imara'' baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo

Anorld Schwarzenegger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Inasemekana Schwarzenegger anaendelea kupona vema hospitalini

Nyota huyo wa filamu mwenye Mmarekani mwenye asili ya Austria na gavana wa zamani wa California mwenye umri wa miaka , 70, alikuwa akifanyiwa upasuaji wa kuwekewa mrija wadamu katika hospitali ya Cedars-Sinai siku ya Alhamisi.

Mrija huo uliwekwa kwa ajili ya kukarabati ule uliowekwa mwaka 1997 uliokuwa na kasoro .

Upasuaji wake siku ya Alhamisi ulidumu kwa muda wa saa kadhaa , kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa TMZ.

Inasemekana Schwarzenegger anaendelea kupona vema na ameripotiwa kusema: '' Nimerejea'' baada ya kuamka kwenye chumba cha upasuaji.

Msemaji wake , Daniel Ketchell, amesema kuwa Schwarzenegger yuko katika "hali nzuri".

Akijibu maswali ya wanahabari ,kansela wa Austria Sebastian Kurz alimtakia "rafikia yake " kuwa na afya nzuri kupitia ujumbe wake wa twittee, akaongeza: " Ninasubiri kwa hamu kukuona tena ."

Schwarzenegger anafahamika zaidi kama mwanamume jasiri katika filamu kama vile the Terminator na Conan the Barbarian.

Alihudumu mihula miwili kama gavana wa California governor kuanzia mwaka 2003 hadi 2011 kabla ya kurejea tena katika filamu za The Expendables.

Mwezi Mei mwaka jana , Schwarzenegger alitunukiwa na tuzo la heshma la - Chevalier de la Legion d'Honneur - medali ya heshma zaidi inayotoyolewa nchini humo kwa kazi yake ya mazingira.

Mada zinazohusiana