Muhindi wa tabaka la chini la Dalit auawa ''kwa kumiliki farasi''

Farasi
Maelezo ya picha,

Katika baadhi ya maeneo nchini India, kumiliki farasi inamaanisha una madaraka na utajiri.

Kijana mmoja mkulima kutoka watu wa tabaka la chini India - la jamii ya Dalit - amepigwa hadi kufa kwasababu anamiliki na kumuendesha farasi

Police katika jimbo la Gujara wanasema kuwa wanaume watatu kutoka tabaka la juu wametiwa nguvuni ili wahojiwe kuhusiana na kisa hicho.

Baba yake marehemu anasema kijana wake huyo alikuwa ameonywa asimuendeshe farasi huyo kwasababu watu matajiri wa tabaka la juu nchio wanaopaswa kuendesha farasi.

Umiliki wa farasi unaangaliwa kama ishara ya mamlaka na utajiri katika baadhi ya maeneo ya India.

Afisa wa ngazi ya juu wa polisi amesema hakuna sababu nyingine ya kuuawa kwa mtu huyo iliyobainika.

Kijana huyo Pradeep Rathod, mwenye umri wa miaka 21, alipatikana akiwa na majeraha makubwapamoja na damu karibu na kijiji cha Timbi katika jimbo la Gujarat Alhamisi usiku .

Farasi wake alipatikana kando yake akiwa ameuawa pia, alisema baba yake marehemu.

Maelezo ya picha,

Ramani ya India kuonyesha lilipo jimbo la Gujarat

Katika malalamiko yaliyowasilishwa kwa polsi, baba yake marehemu alisema mwanae alipenda sana farasi na alikuwa amemnunulia mmmoja.

"Mapenzi ya mwanangu ya farasi yamemsababishia kifo chake," alisema baba yake kulingana na taarifa ya shirika la habari la AFP, ambalo lilishuhudia taarifa hiyo.

'' karibu wiki moja iliyopita, nilipokuwa ninaendesha farasi pamoja na kijana wangu, mmoja wa watu kutoka jamii ya tabaka la juu la Kshatriya alituonya tusiendeshe tena farasi kijijini.

"Alisema kwamba watu wa jamii ya Dalit hawawezi kuendesha farasi , ni watu wa jamii ya Kshatriyas wanaoweza kuendesha farasi.

Pia alitishia kutuua ikiwa hatutamuuza farasi ," ilieleza taarifa ya mashtaka ya baba yake marehemu''.

India ina historia ya mashambulio na ubaguzi dhidi ya watu wa jamii ya Dalit, ambao zamani waliitwa "wasio guswa", ameeleza mhariri wa BBC wa masuala ya Asia Kusini Anbarasan Ethirajan.

Maelezo ya picha,

Jayesh Solanki kutoka jamii ya watu wa tabaka la chini wa jamii ya Dalit pia aliuawa kwa kutazama onyesho densi

Mwezi Oktoba mwaka jana Jayesh Solank kutoka jamii ya Dalit aliuawa alipokuwa amehudhuria densi ya kitamaduni ya jamii ya Hindu katika jimbo hilo la Gujarat.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ghasia dhidi ya Wahindi wa jamii ya Dalit ziliibua maandamano kadhaa nchini India iliyopita

Ubaguzi wenye misingi ya tabaka ni kinyume cha sheria nchini India lakini bado umeshamiri kote nchini humo.