Winnie Mandela alikuwa shujaa au muasi?

A picture taken on April 13, 1986 shows Winnie Madikizela-Mandela, then-wife of South African president Nelson Mandela, addressing a meeting in Kagiso township.

Kifo cha Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, kimezua mjadala nchini mwake namna ambavyo mwanaharakati huyo anastahili kukumbukwa.

Upande wa viongozi wa jadi, pamoja na wafuasi wake, wanataka Winnie akumbukwe kama mwanamke asiyekuwa na hatia.

Huku wengine, haswa wale ambao bado wapo katika mapambano ya awali wakiwa chini ya mwamvuli wa watu weupe wanataka Bi.Winnie Mandela kukumbukwa kama mtu mbaya sana na aliyetenda uasi.

Lakini kwa mtu yeyote ambaye anataka kumuelewa vizuri Bi. Winnie Mandela anapaswa kurejea historia na kuona namna ambavyo alinyanyaswa,kuaibishwa na kuteseka wakati wa mfumo wa ubaguzi wa rangi.

Winnie alikuwa mpigania uhuru, aliyeleta mapinduzi kwa kuwa mapambanaji wa ubaguzi wa rangi, hakuwa mwanaharakati wa kushika silaha na kutegemea mashabiki wa mitandaoni .

Mume wake wa zamani, Nelson Mandela alimwachia watoto wadogo wawili wa kike kuwalea wakati alipofungwa gerezani mwaka 1962.

Bi.Winnie kuitwa mwanaharakati ni haki yake, kwa kuwa ni mwanamke aliyewahi kukakamatwa na kuwekwa gerezani akiwa na nguo zake za kulalia tu, huku polisi wakiwazuia ndugu zake kwenda kumuona na kuzuiwa kuwaona watoto wake.

Maelezo ya picha,

Winnie Madikizela-Mandela alikuwa kati kati ya harakati za kupigania uhuru wa watu weusi

Chumba cha Mateso

Mwaka 1969, Winnie alifungwa gerezani kwa muda wa siku 491, na hakupata msaada hata wa pedi wakati alipokuwa katika siku zake.

Gereza lake halikuwa la kawaida, ila maalum kwa ajili ya kumtesa.

Mateso aliyoyapata gerezani yaliandikwa katika kitabu kiitwacho "491 Days", kinachoelezea kelele ya mwanamke aliyekuwa anapigwa na kuteswa gerezani.

Maelezo ya picha,

Uzoefu wa Winnie Madikizela-Mandela akiwa gerezani ilisimuliwa kwenye kitabu chake cha ' 491 Days'

Baadae wakati ambapo viongozi wengi walipokuwa wanafungwa jela, Bi.Winnie alikuwa mstari wa mbele katika kuongoza harakati hizo akiwa pamoja na hayati Mandela.

Kiufupi ni kwamba Winnie Mandela aliamua kuongoza mapigano ya kutetea watu weusi. Alipobainika kuwa ana ushawishi mkubwa, Winnie alihamishwa katika makazi yake yaliyokuwa katika mji wa biashara wa Johannesburg, kwenda kukaa katika mji mdogo wa Brandfort ambayo ilikuwa ngome imara ya watu weupe.

Hakuruhusiwa kupokea wageni ingawa alikuwa anaweza kusafiri kila siku kwenda posta kupiga simu, ili kuuambia ulimwengu juu ya mfumo wa ubaguzi wa rangi.

Maelezo ya picha,

Klabu ya Soka ya Mandela United ilishutumiwa kwa kufanya uhalifu

Tangu kifo chake kitokee siku ya Jumatatu, kile kilichoandikwa na watu wengi katika mitandao ya kijamii, kinaonesha wazi kuwa kuna baadhi ya watu hawafahamu historia ya Bi. Winnie Mandela.

Kuna wengine wamezungumzia juu ya urembo wake na wengine jitihada zake katika kutetea nchi yake.

Aidha Bi.Winnie pia hakuwa mkamilifu, alikuwa na makosa yake pia.

Aliwahi hukumiwa kwa kosa la udanganyifu na alikamatwa kwa kosa la utekaji nyara.