Wakazi wanaopewa pesa za bure magharibi mwa Kenya
Wakazi wanaopewa pesa za bure magharibi mwa Kenya
Ungefanya nini iwapo ungepewa pesa bure kila mwezi? Je, hii inaweza kuwa njia bora zaidi ya kuangamiza umaskini?
Wakazi wa vijiji 200 magharibi mwa Kenya wamekuwa wakipokea dola 22 za Marekani kila mwezi za kutumia kakidhi mahitaji yao muhimu.
Pesa hizo hutumwa kwa njia ya simu kwa lengo la kuboresha maisha yao.
Baadhi wamewekeza katika kilimo, biashara, karo, ujenzi na hata katika afya.
Lakini mpango huo haujaungwa mkono na wote, baadhi wakiamini kwamba mpango huo utawafanya wanufaika kuzembea.