'Makaburi' ya magari ya Volkswagen nchini Marekani

'Makaburi' ya magari ya Volkswagen nchini Marekani

Kampuni ya kuunda magari ya Volkswagen kutoka Ujerumani ililazimika kununua tena maelfu ya magari ambayo ilikuwa imewauzia wateja baada ya kugunduliwa kuwa na kasoro kwenye injini za dizeli, hatua iliyochangia kutolewa kwa gesi chafu.

Kampuni hiyo ina maeneo 37 ya kuegeshea magari kama hayo, ambayo kawaida hufahamika kama 'makaburi' ya magari.