Afrika Kwa Picha Wiki hii: 30 Machi-5 Aprili

Mkusanyiko wa picha nzuri zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika maeneo mbalimbali duniani wiki hii.

A man lies on the ground carrying a crucifix during a dramatisation of the crucifixion of Jesus Christ to mark Good Friday, heralding the start of Easter celebrations, in Lagos on March 30, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamume alala sakafuni wakati akiigiza kuteswa na kusulubiwa kwa Yesu Kristo wakati wa Ijumaa Kuu mjini Lagos, Nigeria...
A young girl is comforted as she cries during a dramatisation of the crucifixion of Jesus Christ to mark Good Friday, heralding the start of Easter celebrations, in Lagos on March 30, 2018 Haki miliki ya picha AFP
Image caption huku msichana huyu mdogo akituliwa baada yake kuanza kulia wakati wa maigizo hayo.
Worshipers pray during Easter prayers at a Legio Maria African Mission Church in Kibera slum in Nairobi Kenya, April 1, 2018. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hapa, mvulana anaonekana kuwa makini kabisa wakati wa maombi ya Pasaka katika kanisa la Legio Maria mtaa wa Kibera Nairobi Jumapili.
Harun Karanja, the owner of Facebook Curio Shop, uses his mobile phone to access his Facebook account near the Rift Valley town of Mai Mahiu, Kenya March 28, 2018. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Harun Karanja, mmiliji wa duka la sanamu kwa jina Facebook Curio Shop, naye anaonekana akitumia simu yake ya mkono kufungua ukurasa wake wa Facebook katika eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya.
Men work in a construction site in Goma, the capital of North Kivu, eastern Democratic Republic of Congo, April 4, 2018. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamume huyu naye anaonekana akiwa kazini eneo la ujenzi katika mji wa Goma, mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo 4 Aprili, 2018.
Men work in a construction site in Goma, the capital of North Kivu, eastern Democratic Republic of Congo, April 4, 2018 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wengine nao wakiwa kazini kwenye ngazi.
A black and white photograph of the late Winnie Madikizela-Mandela is surrounded by the South African and African National Congress (ANC) flags on a pole at the Old Durban Prison's Human Rights wall as South Africans gather to pay respect to the late high-profile anti-apartheid activist during a candle vigil in Durban on April 2, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Na jijini Durban, Afrika Kusini, picha ya marehemu Winnie Mandela inaonekana wakati wa mkesha wa kumkumbuka mwanaharakati huyo aliyechangia sana juhudi za kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi. Bi Mandela alifariki Jumatatu akiwa na miaka 81...
Members of the ANC Women's League march to commemorate the late South African anti-apartheid campaigner Winnie Madikizela-Mandela, ex-wife of former South African president Nelson Mandela. in Soweto, Johannesburg, on April 4, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake hawa nao wanaonekana wakiimba kumsifu eneo la Soweto, mji ambao Bi Madikizela-Mandela aliishi kwa muda mrefu.
Honour guard members perform during the 43rd Annual Meeting of the Islamic Development Bank Group in Tunis, Tunisia April 4, 2018. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Na katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis maafisa waliandaa gwaride Jumatano wakati wa mkutano wa kila mwaka wa 43 wa Kundi la Benki ya Maendeleo ya Kiislamu.
Gold Coast 2018 Commonwealth Games - Opening ceremony - Carrara Stadium - Gold Coast, Australia - April 4, 2018 - Salome Nyirarukundo of Rwanda carries the national flag during the opening ceremony Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Na nchini Australia, siku hiyo Salome Nyirarukundo wa Rwanda anaonekana akiwa ameibeba bendera ya taifa lake wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola.
dModels present creations by Mark Johnson uring the Accra Fashion Week, in Accra, Ghana, 31 March 2018. The Accra Fashion Week attracts top West African and African designers to showcase their creations from 29 March to 01 April Haki miliki ya picha EPA
Image caption Na Ijumaa, mwanamitindo huyu alipanda jukwaani wakati wa Wiki ya Maonesho ya Mitindo ya Accra.
A woman casts her vote in a ballot box at the polling station in Freetown on March 31, 2018 during the second round of Sierra Leone's presidential election Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumamosi, mwanamke huyu alikuwa akipiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais Sierra Leone.
People celebrate the victory of Julius Maada Bio as new president of Sierra Leone on April 4, 2018 in Freetown, Sierra Leone. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgombea wa upinzani Julius Maada Bio alitangazwa mshindi Jumatano, na wafuasi wake walijitokeza barabarani kusherehekea mji mkuu Freetown.

Picha kwa hisani ya AFP, Reuters, EPA na Getty Images.

Kuhusu BBC