Michezo ya Jumuiya ya Madola : Jamell Anderson na Georgia Jones wavishana pete ya uchumba

Georgia Jones na mpenzi wake wakiwa uwanjani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Georgia Jones na mpenzi wake wakiwa uwanjani

Jumapili itakuwa ni siku ambayo haitasahaulika kwa wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Team England -na hususan kwa wapenzi hao wawili - hawataisahau kamwe.

Baada ya timu ya wanawake ya England kuichapa Msumbiji katika michezo ya Jumuiya ya Madola , Upande wa timu ya wanaume illilaza ile ya Cameroon.

Lakini sherehe zilikua bado hazijaanza uwanjani.

Wakati timu zote mbili zilipokusanyika uwanjani kusherehekea ushindi wao, mchezaji Jones hakufahamu kabisa ni nini kingetokea.

Baada ya ule mkusanyiko wa wachezaji kusambaratika mpenzi wa Jones -Jamell Anderson alikuwa amepiga magoti , huku ameshikilia pete ya uchumba - Jones hakuwa na budi ila kusema ndio nakubali.

Alipoulizwa ni kwanini alichagua eneo hilo kumuomba mchumba Jones, Anderson alisema : "Sote tulifanya juhudi kubwa kuwepo hapa.

"Mpira wa kikapu ni sehemu kubwa ya uhusiano wetu kwa hiyo ilikuwa na maana kubwa kumvisha pete ya uchumba hapa ."

Jones atarejea tena uwanjani Jumatatu wakati ambapo timu ya wanawake ya England itakapokabiliana na Australia katika mchezo wa fainali.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Georgia Jones akionyesha pete yake ya uchumba pamoja na mchumba wake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wachumba wawili wakiondoka uwanjani