Safaricom na Airtel Kenya zaainisha huduma za utumaji wa pesa

Watu milioni 30 Kenya wanatumia simu za rununu Haki miliki ya picha AFP

Kampuni mbili kubwa zaidi za mawasiliano ya simu za mkononi nchini Kenya Safaricom na Airtel zitaanza kusaidia kurahisisha usambazaji wa pesa chini ya mfumo unaowawezesha wateja kuweza kutuma ama kutoa pesa kupitia mtandao usio wa simu yao.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari makampuni hayo ya mawasiliano yamesema kuwa ushirikiano huu wa kuboresha huduma ya kusambaza pesa kwa njia ya simu miongoni mwa wateja inalenga kurahisisha uhamishaji wa pesa baina ya mitandao kwa kuunganisha mifumo ya usambazaji wa pesa kwa njia ya simu.

Wateja wa mitandao yote ya simu wataanza kwa kujisajili katika huduma ya (USSD) nambari ya ujumbe mfupi badala ya ndani ya programu yenyewe huduma hiyo.

'' Wateja wa mtandao wa Safaricom watahitaji kutumia nambari ya ujumbe mfupi kutuma pesa , tofauti na wanapotuma pesa kwa mtumiaji mwingine wa M-Pesa kwa njia ya Menu ya Safaricom ama programu tumizi'', inasema Safaricom.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wateja wa mitandao yote ya simu wataanza kwa kujisajili katika huduma ya (USSD) nambari ya ujumbe mfupi badala ya ndani ya programu yenyewe huduma hiyo.

Mambo unayopaswa kuyafahamu juu ya kuunganishwa kwa huduma za pesa kwa mitandao tofauti ya simu za mkononi:

  • Itapatikana tu kupitia ujumbe mfupi(USSD) si kwa Menu ya safaricom.
  • Wateja wanaweza tu kupokea pesa kwenye wakala wa mitandao walikojisajili.
  • Gharama ya huduma itategemea mtandao.
  • Huduma hii itapatikana tu kwanza kwa wateja wa Safaricom na Airtel, Telecoms ni baadae.
  • Pesa zitakazotumwa zitaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya mpokeaji.

Tayari mtandao wa Safaricom umeanzisha kipengele cha M-Pesa popote kwa ajili ya mfumo huo mpya unaounganisha mitandao ya simu za mkononi kwa ajili ya huduma za usambazaji wa pesa.

Kwa huduma hii makampuni husika yamependekeza kwa pamoja kiwango cha malipo ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mtandao mmoja hadi mwingine yanayotarajiwa kuidhinishwa Benki Kuu ya Kenya (CBK), kulingana na Airtel.

Hata hivyo watumiaji wa huduma ya pesa ya Airtel -Airtel Money hawataweza kupokea pesa zao kutoka kwa wakala wa Safaricom wa M-Pesa ambapo hali itakuwa sawia kwa wateja wa Safaricom.

Airtel inasema kuwa bado inawatarajia wateja wake kupokea pesa kutoka kwa wakala wa mitandao yao kwasababu huduma hakuna wakala wa usambazaji wa pesa chini ya mfumo unaowawezesha wateja kuweza kutuma ama kutoa pesa kupitia mtandao usio wa simu yao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kampuni ya Simu za mkononi ya Safaricom ndio inayotawala soko la pesa kwa njia ya simu za mkononi ikimiliki asilimia 67 ya wakala wa huduma za pesa kwa njia ya simu.

''Kwa ujumla hii inamaanisha kuwa pale mteja wa Airtel Money anapotuma pesa kwa mteja wa M-Pesa salio la akaunti ya mteja wa M-pesa liaonekana mara moja na mteja wa M-pesa anaweza kweda kwa wakala wa M-pesa kupokea pesa ama kuitumia kwa usambazaji mwingine wa pesa kwa njia ya simu ya mkononi.'' Imesema Airtel.

Kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom ndio inayotawala soko la pesa kwa njia ya simu za mkononi ikimiliki asilimia 67 ya wakala wa huduma za pesa kwa njia ya simu(mobile money) ambapo makampuni na taasisi zipatazo 40,000 zinakubali malipo kwa njia ya M-Pesa.

M-Pesa inadhibiti asilimia 80.8 ya soko la hisa kulingana na tathmini ya robo tatu ya mwaka 2017.

Uunganishaji wa huduma za mitandao ya huduma za usambazaji wa pesa kwa njia ya simu ulitambuliwa na utafiti juu ya ushindani kama moja ya mambo muhimu katika kuhakikisha unakuwepo ushindani unaofaa katika soko la pesa kwa njia ya simu za mkononi. Imesema mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya (CA).

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii