Tetesi za soka Ulaya Jumanne 10.04.2018: Mabadiliko yanatarajiwa katika klabu za soka

Meneja wa Chelsea Antonio Konte
Image caption Kazi ya Antonio Konte katika Chelsea imo mashakani na huenda akaihama klabu hiyo msimu huu

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anakabiliwa na tishio tena la kupoteza kazi na Mtaliano huyo anaweza kuondoka kwenye wadhifa huo kabla ya mwisho wa msimu huu. (Mail)

Image caption Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford anasema hakufurahishwa na kiwango cha muda aliopewa kucheza katika Old Trafford

Kocha wa Ujerumani Thomas Tuchel, anayelengwa na timu za Arsenal na Chelsea, amesaini mkataba wa miaka miwili kuwa meneja mpya wa klabu kubwa ya Ufaransa Paris St-Germain kuanzia msimu ujao. (Sportbuzzer - in German)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 20, amekatishwa tamaa na kukosa muda wa kucheza katika Old Trafford na mchezaji huyo wa kimataifa wa England anaweza kuihama klabu hiyo msimu ujao. (Mirror)

Liverpool hawana haja ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 29- Marouane Fellaini kutoka Manchester United, lakini Paris St-Germain (PSG)bado inamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji (Mail)

Image caption Muda wa kocha wa Manchester City Pep Guardiola katika Bayern Munich umechochea utashi wa Buyern kumtafuta meneja mpya

Washindi wa Ligi ya Championi ya Bundesliga Bayern Munich na PSG wanaoongoza Ligi 1 wote wameioamba Chelsea kuendelea kuwapa taarifa iwapo winga Kenedy mwenye umri wa miaka 22- atakuwa tayari kwa uhamisho. Mchezaji huyo wa Brazil kwa sasa ana deni katika Newcastle. (Sky Sports)

Muda wa kocha wa Manchester City Pep Guardiola katika Bayern Munich umechangia kwa kiasi kikubwa haja ya klabu hiyo kumsaka meneja mpya na wanamtafuta Kocha "anayezungumza Kijerumani ", anasema mtaalamu wa soka wa Ujerumani Rafael Honigstein. (BBC Radio 5 live)

Karibu wachezaji nyota 130 wa Ligi ya Primia wanakabiliwa na malipo ya Euro milioni 250 baada ya kuwekeza pesa zao katika mfumo wa kukwepa kulipa ushuru. (Mirror)

Image caption Mshambuliaji wa timu ya West Ham Javier Hernandez, mwenye umri wa miaka 29, yuko tayari kuondoka klabu hiyo msimu huu

Watford wamezipiku Arsenal na Tottenham kwa kusaini mkataba wa thamani ya Euro milioni 1.5 kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa timu ya England ya vijana Ben Wilmot, mwenye umri wa miaka 18 . (Sun)

Mshambuliaji wa timu ya West Ham Javier Hernandez, mwenye umri wa miaka 29, yuko tayari kuondoka klabu hiyo msimu huu wa majira ya joto huku raia huyo wa Mexico akitafuta timu ya soka ya kuichezea. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aston Villa wanamuwinda mchezaji wa safu ya kati wa West Brom Jake Livermore, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ana matumaini ya kuwa katika kikosi cha timu ya England ya Kombe la Dunia.

Mchezaji wa timu ya RB Leipzig- Mfaransa mwenye umri wa miaka 19-anayecheza katika safu ya ulinzi Dayot Upamecano anasema "ana ndoto za " kucheza katika timu za Real Madrid, Barcelona ama ​​Manchester United siku moja (Telefoot - in French)

Aston Villa wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya kati wa West Brom Jake Livermore, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ana matumaini ya kuwa katika kikosi cha timu ya England ya Kombe la Dunia. (Mail)

West Brom inaweza kumpoteza mshambuliaji Salomon Rondon mwenye umri wa miaka 28 watapuuza matakwa ya raia huyo wa Venezuela ambaye ameongeza kipengele cha Euro milioni 16.5 kwenye mkataba wake. (Mirror)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright anasema meneja maneno ya Arsene Wenger yalimfanya ajihisi mwenye "kuwa anga za juu", huku yale ya meneja wa zamani wa Gunners George Graham yakimfanya ajihisi "anakimbilia msalani". (BBC Radio 5 live)

Mada zinazohusiana