Daktari wa kienyeji aliyewalaghai wanawake Guinea afungiwa

False pregnancy Haki miliki ya picha BBC's Alhassan Sillah
Image caption Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.

Mwanamke mmoja Guinea ambaye aliwauzia dawa za kienyeji kwa wagumba, akiwaambia kuwa wangepata mimba, amefungiwa miaka mitano.

N'na Fanta Camara alitengeneza dawa ya kienyeji ambayo ilisababisha matumbo yao kufura na kuonekana kuwa ni wajawazito.

Daktari huyo wa kienyeji anasemekana kuwalaghai zaidi ya wanawake 700 akiwa toza fedha nyingi kwa matibabu.

Mwandishi wa BBC Alhassan Sillah aliyopo jiji la Conakry , anasema waathirika waliojitokeza mahakamani walikasirika kwamba hakupata hukumu nzito.

Camara,alipatwa na hatia ya kumuiga daktari kwa kuwapatia wanawake hao dawa zilizowadhuru na zilizoweka maisha yao hatarini.

Aliagizwa kulipa fidia ya dola za Marekani 165,000

Washirika wengine wawili walihukumiwa kwa mashtaka hayo pia na kuhukumiwa kifungo cha muda wa miaka tatu hadi minne gerezani.

Haki miliki ya picha BBC's Alhassan Sillah

Kutokana na huduma hizo wagonjwa walilipa dola 33 kwenye nchi ambayo kipato cha kila mwezi kinakadiriwa kuwa dola 48.

Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.

Mwaka 2006 shirika la afya duniani lilisema kuwa asilimia 80 ya waafrika walitumia matibabu ya kienyeji.

Mada zinazohusiana