Idara ya Uhamiaji Tanzania imekanusha shutuma za kutumika kisiasa katika kufanya kazi zake
Idara ya Uhamiaji Tanzania imekanusha shutuma za kutumika kisiasa katika kufanya kazi zake
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imekanusha shutuma kwamba inatumika kisiasa katika kufanya kazi zake. Shutuma hizi zimekuja baada ya watu wanaojulikana kuwa wakosoaji wa serikali kuitwa na idara hiyo na kuhojiwa juu ya uhalali wa uraia wao. Lakini hata hivyo, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Ali Mtanda amemwambia mwandishi wetu Sammy Awami kwamba wanachokifanya ni kufanyia kazi tu taarifa za walakini wa uraia wa watu fulani zinazoletwa na wananchi