Hali si shwari, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati ameyashutumu makundi ya wapiganaji yanayopambana na walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Rais Faustin-Archange Touadera amesema makundi hayo yamekuwa wakifanya uhalifu, hali iliyosababisha watu wengi kukamatwa mateka.

Siku ya Jumapili Vikosi vya jeshi vya Umoja wa Mataifa vilianza operesheni yake kuwanyang'anya silaha wanamgambo ambao wanadhibiti baadhi ya maeneo katika mji mkuu wa nchi.

Mmoja wa walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mapema jana mamia ya waandamanaji wenye hasira waliilaza miili ya watu 16 mbele ya Ofisi ya vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa mjini Bangui.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema vikosi vyao vimekuwa vikilenga makundi ya wahalifu na kukanusha taarifa kwamba wamekuwa wakishambulia raia.

Mada zinazohusiana