Wanasayansi wagundua aina mpya ya chandarua kinachoimarisha kinga dhidi ya Malaria

mbu malaria Haki miliki ya picha Science Photo Library

Kila mwaka takriban watu nusu milioni hufariki kutokana na Malaria. Suluhu moja rahisi ni kutumia vyandaruwa vya kujikinga na mbu vilivyotibiwa na viuatilifu vinavyoua vidudu.

Lakini kadri miaka inavyosogea, kumezuka tatizo jipya. Mbu wameweza kupambana na makali ya kemikali.

Wanasayansi wamepata suluhu, wamegundua kwamba vyandarua hivyo vikitumika pamoja na dawa ya viuatilifu (inayoua vidudu) inayojulikana kama Piperonyl Butoxide, inazuia mbu kuweza kupambana na viuatilifu, na hivyo kupunguza maambukizi ya malaria kwa zaidi ya theluthi moja.

Dkt Natacha Protopopoff, aliyeongoza majaribio ya aina mpyaya chandarua waliogundua ina iwezo wa kuimarisha kinga dhidi ya Malari, ameiambia BBC kwamba huenda neti hizo zikapunguza kwa kiwango fulani viwango vya ugonjwa wa Malaria.

"Majaribio haya ya aina hii mpya ya neti yanadhihirisha kupungua vizuri kwa maambukizi ya malaria.

Ilipunguza viwango kwa 44% katika mwaka wa kwanza, na pia 33% katika mwaka wa pili kwasababu vyandarua vimetibiwa kiwandani na hivyo kuruhusu kemikali hiyo kusalia katika chanadarua kwa miaka mitatau au kutumiwa katika majaribio."

Haki miliki ya picha Science Photo Library

Ugunduzi huo umefanywa na timu kutoka taasisi ya London School of Hygiene and Tropical Medicine, katika utafiti wao walioufanya kwa miaka miwili uliohusisha zaidi ya watoto elfu 15 nchini Tanzania.

Shirika la Afya duniani kwa sasa linashauri matumizi ya vyandarua hivyo vipya.

Mambo 10 kuhusu Malaria:

  • Malaria husababishwa na vimelea vinavyosambazwa baada ya mbu walioambukizwa navyo kuwauma binaadamu
  • Takriban nusu ya idadi ya watu duniani wamo katika hatari ya kuugua malaria
  • Watoto walio chiniya umri wa miaka 5 wamo katika hatari kubwa ya kuugua malaria
  • Viwango vya watu wanaokufa kutokana na malaria vinapungua
  • Kutambua na kutibu mapema wagonjwa wanaougua Malaria kunazuia vifo
  • Wasiwasi unaongezeka kuhusu uwezo wa vimelea kupambana na makali ya dawa za kutiba malaria - artemisinin
  • Kulala chini ya vyandarua vilivyotibiwa vya kujikinga na mbu, kunakinga maambukizi ya malaria
  • Kupuliza dawa ndani ya nyumba ndio njia muafaka ya kupnguza haraka maambukizi ya Malaria
  • Wanawake waja wazito ndio wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa malaria
  • Malaria inasababisha athari kubwa kiuchumi katika nchi maskini
Haki miliki ya picha Getty Images

Matokeo yanapokewaje Tanzania?

Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la afya la Lancet.

Matokeo yanayoonekana kuwa mazuri ya majaribio ya vyandarua hivi Tanzania tayari yamechangia shirika la afya duniani WHO kupendekeza vitumiwe pakubwa.

Dkt. Govella is Mwanasayansi mkuu wa utafiti na mkuu wa idara ya utafiti wa Malaria katika Taasisi ya Afya Ifakara, anasema:

"Uwezo wa mbu kupambana na makali ya viuatilifu vinavyotumika katika vyanarua umekuwa ni changamoto kubwa katika vita vya kupambana na malaria duniani.

Nina matumaini kwamba vyandarua vya kujikinga na mbu vinavyojumuisha kemikali stahili (piperonyl butoxide) iliyogunduliwa hivi karibuni vitatusaidia kuendeleza kazi nzuri iliopo sasa kutokana na matokeo ya matumizi ya vyandaruwa vilivyotibiwa."

Matumizi ya vyandaruwa vilivyotibiwa vya kujikinga na mbu imesaidia kupunguza idadi ya vifo vya malaria kwa miaka kadhaa, lakini hatua zimekwama hivi karibuni katika kupambana na ugonjwa huo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii