Simba jike na watoto wao wadaiwa kufa kwa sumu Uganda

Uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha kifo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha kifo

Simba jike watatu na watoto wao wanane wamekutwa wamekufa kutokana na kinachoshukiwa kuwa sumu.

Wanyama hao wamekutwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Queen Elizabeth kusini magharibi mwa Kampala

Mamlaka ya hifadhi ya Uganda, imesema kuwa simba hao wanashukiwa kuwa walililishwa nyama yenye sumu.

Uchunguzi kuhusu tukio hilo umeanza

Msemaji ameiambia BBC kuwa iligundulika siku ya Jumatano, umbali wa mita 100 kutoka kwenye kijiji kimoja cha uvuvi.

Wanyama hao hawakuonekana kama walikuwa na majeraha mwilini.

Idadi ya simba kwenye hifadhi ya Queen Elizabeth inakadiriwa kuwa 100, kati ya hao karibu 400 wako hai nchini Uganda.

Hifadhi za Uganda ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya mapato yanayotokana na utalii. Lakini mara kadhaa kumekuwa na mvutano kati ya wahifadhi na wananchi.