Binti mfalme atupwa jela Dubai

runway princess,Dubai
Image caption Mfalme Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum, babake Sheikha Latifa

Watetezi wa haki za binaadamu walioko mjini London wametoa wito kwa serikali ya Falme za kiarabu kutoa maelezo ya nini kilichomkuta bintimfalme ambaye amerusha video akieleza namna babake, mfalme wa Dubai , anavyotishia maisha yake .

Kikundi hicho kimewekwa kizuizini huko Dubai kimesema kuwa Latifa al-Maktoum alikuwa akijaribu kutoroka himaya ya babake kwa kutumia jahazi lililokuwa na linapeperusha bendera ya Marekani, baada ya kuingia katika bahari ya kimataifa mwezi uliopita wakiwa na walinzi wa bahari ya Hindi.

Inaarifiwa kuwa Sheikha Latifa na watu wengine watano walichukuliwa kwa nguvu kutoaka katika jahazi hilo na kuhojiwa kwa muda wa wiki mbili. Na watu wengine waliachiliwa bila mushkeli ingawa binti huyo hajulikani halipo.

Mpaka sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa kutoka falme za kiarabu ama nchini India. Katika mkanda wa video uliorekodiwa kwa muda wa dakika arobaini na kuwekwa katika mmmmitandao ya kijamii, Sheikha Latifa ameeleza kuwa alikuwa amewekwa kizuizini chini ya amri ya babake, Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum, kwa kujaribu kumsaidia dadake aliyeasi.