DRC yasusia mkutano wa Umoja wa mataifa Geneva ulioandaliwa kuisaidia nchi hiyo

A Congolese man holds his child after he crossed the border from the Democratic Republic of Congo (DRC) to be refugees at Nteko village in western Uganda on January 24, 2018. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya wakimbizi kutoka DRC wamvuka mpaka kuingia nchini Uganda

Serikali ya Congo imekataa kuhudhuria mkutano huo wa kuchangisha fedha za msaada kwa janga linaloshuhudiwa nchini ikisema Umoja wa mataifa umetilia chumvi ukubwa wa tatizo lililopo.

Katika mkutano maalum mjini Geneva Uswizi, Umoja wa Mataifa ulikuwa unatarajia kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinaadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 5 wamelazimika kuyatoroka makazi yao kwasababu ya mapigano katika sehemu tofauti za nchi hiyo kubwa.

Lakini serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo wa ufadhili ikisema kwamba hali inafanywa kuwa mbaya wakati ni kinyume.

Umoja wa Matiafa umejibu kwa kutangaza majanga ya kibinadamu nchini humo kuwa kiwango cha tatu - kiwango cha dharura cha juu zaidi.

"Hali imefikia kiwango cha Yemen na Syria kwa namna ambavyo watu wanahitaji msaada, ameeleza Jan Egeland, mkuu wa zamani wa Ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulikia maswala ya dharura ambaye sasa anaongoza baraza la wakimbizi la Norway pia hivi karibuni alikuwa DRC.

Janga la DR Congo kwa takwimu

  • Watu milioni 13 wanahitaji msaada wa kibinadamu
  • Tarkiban milioni 4.5 wamekimbia makazi
  • Zaidi ya watu milioni 7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula
  • Watoto milioni mbili waka hatirini kukosa chakula - hii ni asilimia 12 za kesi hizo duniaini

Chanzo: Umoja wa Mataifa

Haki miliki ya picha NRC/CHRISTIAN JEPSEN

Mkutano huo umedhamiria kuchangisha dola bilioni 1.7 kupunguza uzito wa inachotajwa na Umoja wamataifa kuwa ni janga kubwa la kibinaadamu nchini Congo.

Mpaka sasa serikali ya DRC haijajibu mwaliko wa Umoja wa mataifa ikisema taasisi hiyo kuu imetilia chumvi hali halisi nchini na ukubwa wa tatizo lililopo.

Mashirika ya misaada yanasema watu milioni tano wamelazimika kuyatoroka makazi yao kutokana na ghasia, mapigano, njaa na ukosefu wa utulivu na kwamba maelfu ya raia wa Congo wamelazimika kutafuta hifadhi magharibi mwa Uganda.

Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu ndani ya DRC wamekumbwa wasiwasi kutokana na hatua hiyo ya serikali kususia mkutano huo mkuu mjini Geneva.

Image caption Kumeshuhudiwa ghasia na maandamano nchini kumshinikiza rais Joseph Kabila aondoke madarakani

Wasiwasi wa aina hiyo pia umetolewa na baadhi ya raia wanaosema kwamba wataendelea kuteseka bila ya msaada wa jumuia ya kimataifa.

Je kuna hasara ganikwa serikali hiyo kukataa kuhudhuria mkutano wa Geneva?

Mashirika ya misaada yanasema DRC inateseka katika janga kubwa lenye uzito la kibinaadamu lililosahaulika kwa muda mrefu.

Kuna watu milioni 13 wanaohitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2 wanaugua utapia mlo mbaya, na watu milioni 4.5 wamepoteza makazi yao.

Lakini tathimini hii ya mashirika ya misaada imeiudhi serikali ya DRC.

Inatizama kiwango cha daraja la tatu kilichowekwa cha hali ya janga hilo kuwa kama tusi.

Haki miliki ya picha NRC/CHRISTIAN JEPSEN
Image caption Mashirika ya misaada yanasema watu milioni 13 wanahitaji usaidizi: miongoni mwao watoto milioni 2

Na ndio sababu ikachukua hatua hii ambayo haikutarajiwa ya kususia mkutano wa Geneva.

Hata hivyo,maafisa wa Umoja wa mataifa wanatumai kwamba wanadiplomasia wa Congo watabadili uamuzi wao na wahudhurie mkutano huo leo.

Ni wazi kwamba mkutano wenyewe utaendelea licha ya chochote kile kitachotokea, wanaharakati wanasema maisha ya mamilioni ya watu yamo hatarini.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii