Hatua ya Trump: Marekani na washirika wake watekeleza mashambulio Syria

US President Donald Trump addresses the nation on the situation in Syria April 13, 2018 at the White House in Washington, DC. Trump said strikes on Syria are under way. Haki miliki ya picha AFP

Mataifa ya Marekani ,Ufaransa na Uingereza yamefanya mashambulio wakilenga vituo vitatu huko Syria kama adhabu kwa madai kwamba utawala wa Raisi Bashar alsaad,ulitumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.

Taarifa zinasema milio ya milipuko imesikika katika maeneo kadhaa ya miji Damascus na Homs.

Katika taarifa yake rais Trump amedai vituo vilivyo lengwa vinahusiana na utafatiti uhifadhi na utengenezaji wa silaha za kemikali.

Rais Trump ameongeza kusema "Na kwamba marekani iko tayari kuendeleza mashambulio hayo hadi utawala huo wa Syria utakapokoma kabisa kutumia silaha za kemikali."

Pia ameilaumu Urusi kwa kutoidhibiti mshirika wake Syria kutotumia silaha hizo kama ilivyoahidi 2013.