Marekani yaionya Syria: Tutawashambulia tena

Tomahawk fired from USS Monterey Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kombora la Tomahawk likirushwa kutoka USS Monterey

Rais wa Marekani Donald Trump ameiambia serikali ya Syria akisema Marekani iko tayari kuishambulia tena ikiwa itafanya shambulizi lingine la kemikali.

Onyo hilo lilikuja bada ya Marekani, Uingereza ba Ufaransa kushambulia vituo vitatu kujibu shambulizi linaloshukiwa kuwa la kememikali kwenye mji wa Douma wiki moja iliyopita.

Syria inakana kufanya shaambulizi lolote la kemikali na badala yake inasema kuwa lilifanywa na waasi.

Kura iliyoletwa na Urusi kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataiafa, kulaani mashambulizi yaliyoongoznwa na Matekani ilikataliwa.

Mashambulizi hayo ndiyo makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad, yaliyofanywa na nchi za magharibi katika kipindi cha miaka saba nchi hiyo imekuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege ya Uingereza ya Tornado GR4 ikiondoka nchini Cyprus kwenda kushambulia

Marekani, Uingereza na Ufaransa wamewapa azimio jipya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wakitaka kufanya uchunguzi huru kuhusu matumaini ya silaha za kemikali nchini Syria.

Mipango ya awali ilikuwa imezimwa na Urusi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amelaumu ukosefu wa ushirikiano kutoka Urusi kwa kuchagua kufanya mashambulizi ya kijeshi akisema hawakuwa na njia nyingine.

Uchunguzi ulikuwa ukiendelea?

Wachunguzi kutoka shirika huru linalopambana na silaha za kemikali OPCW tayari wametumwa nchini Syria na wanatarajia kuzuru Douma wikendi hii.

Lakini OPCW hawatataka kutangaza ni nani alihusika kwenye shambulizi hilo kitu ambachio Marekani, Uingereza na Ufaransa wangetaka kifanyike

Azimio hilo jipya pia linaitaka OPCW kutoa ripoti yao ndani ya siku 30.

Ni kipi kilifanyika kwenye Umoja wa Mataifa?

Mkutano wa dharura alifanywa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi ulisababisha majibizano makali.

Urusi ilitaka mashambulizi hayo kulaaniwa.

Kati ya nchi 15 ni China na Bolivia zilizopiga kura ya kuunga mkono azimio hilo la Urusi.

Mjumbe wa Urusi Vassily Nebenzi alisoma taarifa kutoka kwa Putin iliwalaumu Marekani, Uingereza na Ufaransa kwa kuchukua hatua bila ya kuongoja matokeo kutoka kwa OPCW.

Syria inasemaje?

Mjumbe wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa alisema Marekani, Uingereza na Ufaransa ni waongo ambao wanatumia Umoja wa Mtaiafa kuingilia nchi nyinngine na kwa ukoloni.

Siku ya Jumamosi, jeshi la Syria lilitangaza kuwa eneo la mashariki la Ghouta ambapo kuna mji wa Douma limeondolewa waasi wote na kutwaliwa.

Image caption Ramani