Mwanamuziki Koffi Olomide amealikwa tena nchini Kenya

Koffi Olomide amesema hakukusudia kumpiga teke mwanamke huyo
Image caption Koffi Olomide amesema hakukusudia kumpiga teke mwanamke huyo

Mwanamuziki Koffi Olomide ametangaza kuwa na onyesho la muziki mwezi huu tarehe 24 nchini Kenya.

Onyesho hili litakuwa la kwanza nchini Kenya tangu alivyokataliwa kuingia nchini humo Julai 2016 baada ya kumdhalilisha mmoja wa wanenguaji wake .

Koffi amesema hayo katika ujumbe wa video kwamba amealikwa kufanya onyesho katika mkutano wa taifa la Kenya ambao utajumuisha viongozi 47 wa nchi hiyo ambao ni mjumuisho wa rais na viongozi wa juu wa serikali.

Mwanamuziki huyo Koffi Olomide anayefanya muziki wa lingala mwenye umri wa miaka 61, aliomba radhi mara kadhaa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha nchini Kenya kwa kumpiga mnenguaji wake.

Katika tangazo la video lilowekwa kwenye mtandao wa Youtube inayotambulisha ziara yake mpya ya muziki,Koffi ameonekana akiwaambia mashabiki wake wa Kenya kuwa anawapenda sana na anawakumbuka sana

Tukio lililomtia utatani lilirekodiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ambako alikuwa amewasili kwa tamasha lilopangwa kufanyika nchini Kenya.

Wengi wa Wakenya walimkashifu vikali kitendo hicho huku maoni katika mitandao ya kijamii, kutpita mada ya #KickKoffiOlomideBackToCongo kwenye Twitter walipendekeza afurushwe kutoka Kenya.

Olomide aliwahi kujitetea kwa kusema kuwa alikuwa akijaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.

Mada zinazohusiana