Jumuiya ya Madola: mambo 7 ya kufahamu

Karibu theluthi ya watu duniani ni wanachama wa Jumuia ya madola Haki miliki ya picha PA
Image caption Karibu theluthi ya watu duniani ni wanachama wa Jumuia ya madola

Viongozi wa jumuia ya madola wanakutana London yafuatayo ni mambo saba ya kufahamu:

1) Karibu theluthi ya watu duniani ni wanachama wa Jumuia ya madola.

Takriban watu bilioni 2.4 kati ya bilioni 7.4 wanaishi kwenye nchi wanachama 53 za jumuia ya madola wengi wao wakiwa chini ya miaka 30.

nchi kubwa kwa idadi ya watu ni India, ambayo ina watu nusu ya idadi kamili.lakini wanachama 31 wa jumuia hiyo wana idadi ya watu milioni 1.5 au chini yake.

2.Baadhi ya wanachama hawakuwa koloni la Uingereza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rwanda ilitawaliwa na Ujerumani na Ubelgiji na si Uingereza

Rwanda na Msumbiji walijiunga uanachama mwaka 2009 na 1995 mtawalia, kwa pamoja hazikuwa na historia ya kutawaliwa na Uingereza.

jumuia hiyo pia iliwahi kupoteza wanachama wake huko nyuma.Robert Mugabe aliiondoa Zimbabwe kwenye jumuia mwaka 2003 baada ya ripoti za ushindi wa udanganyifu wakati wa uchaguzi.

Pakistani iliondolewa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1999 na kurejeshwa tena baada ya miaka minne na nusu.Na Afrika Kusini ilijiondoa mwaka 1961 baada ya kukosolewa na wanachama wa jumuia dhidi ya sera zake za kibaguzi.Afrika Kusini ilirejea tena mwaka 1994

Nchi ya mwisho kuondoka kwenye jumuia ilikuwa Maldives mwaka 2016.

3.Malkia ni Kiongozi wa nchi katika nchi 16 pekee.

Nchi za jumuia ya madola ni jamuhuri na sita-Lesotho,Swaziland,Brunei Darussalam,Malaysia,Samoa Tonga, wana mfumo wa utawala wao wa kifalme.

Image caption Malkia ni Kiongozi wa Jumuia

4) Jumuia ya madola ina idadi ya wanachama wanaofikia robo ya watu duniani.

Nchi kubwa kabosa, Canada, ya pili kwa uchumi mkubwa.India na Australia ni kubwa pia.lakini nchi nyingi ni ndogo,kama vile Nauru, Samoa, Tuvalu ,Vanuatu, Dominica na Antigua na Barbuda eneo la visiwa vya Caribbean.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tonga ina Kiongozi wake wa kifalme-Tupou wa 6 (katikati)

Ni kubwa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Canada ni kubwa

5) Ilibadili jina lake

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Viongozi wa nchi za jumuia ya madola pia walikutana London mwaka 1969

Jumuia mpya ya madola iliundwa mwaka 1994.Watu walikuwa wakiiongoza jumuia hii, Mfalme George wa sita na Malkia Elizabeth wa pili.lakini nafasi hii si ya kurithi, ingawa mwana mfalme wa Wales anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo atakapokuwa mfalme.

Jumuia hii ilikua na wanachama kama Australia, Canada, India, New Zealand, Pakistan, Afrika Kusini, Sri Lanka na Uingereza, ambazo ziliunda ''jumuia huru'' ya nchi zilizo huru.

Jumuia ya madola haikuwa na katiba mpaka ilipokuwa na mkataba wake mwaka 2012,ambayo ilizitaka nchi wanachama kuheshimu demokrasia, usawa wa jinsia,maendeleo endelevu na amani na usalama

Jumuia ya madola imekuwa ikikosolewa kwa kuwa kilabu cha ukoloni na kutokuwa na ushawishi.Gambia ilitangaza kujitoa mwaka 2013 wakikiita na chombo cha ''ukoloni mamboleo''

6) Uingereza ina uchumi mkubwa wa jumuiya ya madola

Image caption Uingereza inaongoza kwa uchumi mkubwa ndani ya jumuia

7) Kuna zaidi ya jumuiya ya madola moja

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jumuia ya madola ya nchi huru ilikutanza hivi karibuni mjini Minsk nchini Belarus

Usisahau kuwa jumuia ya nchi zinazozungumza kifaransa, La Francophonie na kuna jumuia ya madola ya nchi huru, iliyoundwa mwaka 1991 na wanachama wa jumuia ya nchi za kisovieti.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii