Akamatwa kwa kumtupa mwanawe kutoka juu ya paa la nyumba Afrika Kusini

Mtoto huyo amechukuliwa kutoka kwa uangalizi wa mamake Haki miliki ya picha South African Police service Facebook
Image caption Mtoto huyo amechukuliwa kutoka kwa uangalizi wa mamake

Raia mmoja wa taifa la Afrika Kusini ameshtakiwa mahakamani kwa unyanyasaji wa mtoto baada ya kumtupa mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja kutoka juu ya paa la nyumba yake wiki iliopita.

Mashtaka yake yalipunguzwa kutoka kwa jaribio la kutaka kuua , kulingana na mwandishi mmoja wa shirika la habari la eNCA aliyetuma ujumbe wa Twitter.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 alichukuliwa katika kanda ya video akimrusha mtoto huyo wakati wa maandamano dhidi ya uvunjanji wa mitaa ya mabanda katika mji wa pwani wa Port Elizabeth.

Huwezi kusikiliza tena
Mtoto mwenye umri wa miaka 6, amebuni programu ya mchezo wa kompyuta

Gazeti moja la eneo hilo lilituma ujumbe wa Twitter wa picha ya afisa wa polisi akimkamata.

Polisi walikuwa wakivunja vibanda 150 katika makaazi ya Joe Slovo ambayo wanasema yalijengwa katika ardhi iliokaliwa kinyume na sheria.

Mtu huyo ambaye nyumba yake ndio iliokuwa haijavunjwa , alisaidiwa kupanda juu ya paa na mwanamke aliyeripotiwa kuwa mama wa mtoto huyo.

Alikuwa juu ya paa hilo kwa takriban dakika tano kabla ya kumtupa huku wakaazi wengine wakipiga kelele ''mtupe, mtupe, mtupe'' kulingana na jarida la Herald.

Mtu huyo ambaye bado hajaulizwa kujitetea amewekwa kizuizini

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii