IMF lakadiria uchumi kukuwa duniani 2018, lakini Afrika iko wapi?

Sekta ya kilimo iliimarika kwa sehemu kubwa ikishinikizwa na uwekezaji wa miundo msingi na uzalishaji wa vyakula.
Image caption Sekta ya kilimo iliimarika kwa sehemu kubwa ikishinikizwa na uwekezaji wa miundo msingi na uzalishaji wa vyakula.

Shirika la fedha la kimataifa IMF limesema 2018 ndio mwaka utakaoshuhudia ukuwaji mkubwa wa kiuchumi duniani tangu 2011.

Hatahiyo uwezekano wa ukuwaji huo kwa mataifa yanayoendelea kusini mwa jangwa la Sahara hautokuwa rahisi katika miaka mitano ijayo.

Je ni kwanini?

IMF linakadiria kwamba ukuwaji wa pato jumla la nchi katika mataifa yaliopo kusini mwa jangwa la Sahara utaongezeka taratibu kati ya 2018 na 2019 kwa asilimia 3.4% hadi 3.7%, mtawalaia, huku bei za bidhaa zikipanda.

Shirika hilo linalotoa mikopo kwa mataifa duniani hatahivyo linasema lina matumaini kuhusu uwezekano huo wa ukuwaji wa uchumi likitabiria ukuwaji wa hadi 3.9% mwaka huu kutoka 3.8% mwaka 2017 .

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ukuwaji wa uchumi katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sagara umekuwa kwa asilimia 2.4 baada ya kushuka kwa 1.3 mnamo 2016

Limeonya hatahivyo kwamba kasi hiyo huenda isiwe ya muda mrefu katika mataifa hayo yanayoendelea.

Ni kwanini kuna uwezekano mgumu wa ukuwaji wa uchumi kwa Afrika:

Kwa mujibu wa benki kuu ya dunia - Ukuwaji wa uchumi katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sagara umekuwa kwa asilimia 2.4 baada ya kujivuta na kushuka kwa kasi kubwa mnamo 2016 kwa asilimia 1.3

Ukuwaji huu unatokana na kufufuka kwa uchumi wa mataifa ya Angola, Nigeria, na Afrika kusini - mataifa makubwa kiuchumi katikia eneo hilo.

Kuimarika kwa bei za bidhaa pia kumeisaidia hali , pamojana mazingira mazuri yakifedha duniani na kupungua kwa gharama ya maisha hatua iliyochangia kuongezeka kwa mahitaji ya watu.

Huwezi kusikiliza tena
Uchumi waathiri sekta za kilimo na viwanda Tanzania

Hatahivyo ukuwaji ulikuwa mdogo kinyume na ilivyotarajiwa wakati eneo linaendelea kuathirika na uwekezaji na uzalishaji duni wa bidhaa nchini.

Kuna onyo kuhusu hatari zilizopo katika siku za usoni, hatari zinazoweza kusababisha uchumi kuanguka chini ya utabiri wa IMF.

Viwango vya madeni katika sekta binafsi na hata za serikali vipo juu mno.

Hili linaweza kusababisha mataifa yanayochukuwa mikopo kushindwa kuyalipa madeni wakati viwango vya riba vinapanda kutokana na athari za mzozo wa kiuchumi.

Madeni ya serikali yanaendelea kuongezeka katika eneo zima ikilinganishwa na mwaka 2016, wakati mataifa yanachukuwa mikopo kufadhili uwekezaji wa umma.

Nini kifanyike kushinikiza ukuwaji?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwanauchumi mkuu wa IMF Maurice Obstfeld

Kwa mujibu wa mtazamo wa kiuchumi duniani - World Economic Outlook, wasiwasi kuhusu hatari ya mfumo wa fedha, uwezekano wa mageuzi ya sera za biashara, wasiwasi wa kisiasa kieneo na hata tabia nchi kunazidisha hatari za kiuchumi kimataifa.

Shirika la IMF linapendekeza kuwa kuna haja ya kupanua uchumi kando na kutegemea usafirishaji wa bidhaa katika mataiafa ya nje kama inavyofanyika miongoni mwa mataifa mengi yanayoendelea.

Ukuwaji umeshuhudiwa katika mataifa yanayosafirisha vyuma.

Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Sekta ya uchimbaji madini inatajwa kuimarika

Hatua inayodhihirisha kuimarika kwa sekta ya uchimbaji madini huku kukishuhudiwa kupanda bei za vyuma.

Sekta ya kilimo iliimarika kwa sehemu kubwa ikishinikizwa na uwekezaji wa miundo msingi na uzalishaji wa vyakula.

IMF linatoa wito kwamataifa kupatiliza ukuwaji unaoshuhudiwa katika muda mfupi ujao kuidhinisha sera na mageuzi yatakayoimarisha uwezekano wa ukuwaji mkubwa zaidi na unaoshirikisha pande zote, na kuweka mikakati madhubuti ikiwemo kuimarisha mifumo ya fedha na kuongeza ushirikiano wa kimataifa kabla ya uchumi kudorora.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii