Ali Kiba afunga ndoa na mpenziwe wa Kenya

Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya
Image caption Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya

Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya.

Harusi hiyo ya kukata na shoka iliofanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum ilihudhuriwa na rafiki wa mwanamuziki huyo Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Haki miliki ya picha Instagram/dizzim

Mwanamuziki huyo wa wimbo wa Seduce me aliisafirisha familia yake mjini Mombasa siku moja kabla ya kumuoa mchumba wake.

Ni watu wachache pekee walioalikwa katika harusi hiyo iliodaiwa kufanyika kisiri.

Huwezi kusikiliza tena
Zari: 'Diamond alinidhalilisha sana'

Duru zimearifu kwamba sherehe nyengine ya kukata na shoka inatarajiwa kufanyika Aprili 26 mjini Dar es Salaam.

Mada zinazohusiana