Mlimbwende Agnes Masogange kutoka Tanzania aaga dunia

Mlimbwende wa Tanzania Agnes masogange ameaga dunia Haki miliki ya picha Dick Sound
Image caption Mlimbwende wa Tanzania Agnes masogange ameaga dunia

Mlimbwende mnogesha video za muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Agnes Gerald Alias Masogange ameaga dunia.

Kulingana na wakili wa msanii huyo, alifariki siku ya Ijumaa mwendo wa saa kumi jioni.

Inadaiwa kuwa aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Mama ngoma katika eneo la Kindondoni.

Kulingana na shemeji yake Dick Sound, mazishi yake yatafanyika siku ya Jumatatu nyumbani kwao huko Mbeya.

Mlimbwende huyo aliyekuwa na umri wa miaka 28 alinusurika kifungo cha miaka mwili baada ya hakimu wa mahakama ya Kisitu kumpata na hatia ya utumizi wa mihadarati.

Tarehe 6 Aprili hakimu mkaazi alimuagiza kulipa faini ya Tsh.1.5m la sivyo ahudumie kifungo cha miaka miwili.

Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Agnes Masogange

Lakini mwezi Julai 2013 alikuwa miongoni mwa raia wawili wa Tanzania waliokamatwa mjini Johannesburg, Afrika Kusini kwa madai ya kumiliki mihadarati.

Masogange alipata umaarufu 2010 wakati aliposhiriki katika kanda ya video ya wimbo wa msanii Belle9.

Kanda hiyo ya video ilijulikana kwa jina Masogange.

Alionekana katika kanda nyengine za video kabla ya kuwa mlimbwende aliyejiimarisha hatua iliompatia umaarufu mkubwa katika tasnia ya ulimwende wa kunogesha kanda za video nchini Tanzania.

Mada zinazohusiana