Je unaweza kuishi bila kutumia plastiki?

Inawezekana kutotumia plastiki
Image caption Inawezekana dunia ikaacha kutumia plastiki ili kunusuru mazingira

Plastiki zimetajwa kuathiri mazingira ya bahari kwa kiasi kikubwa pamoja na viumbe hai wa baharini.

Maslahi ya kibiashara yamekuwa kikwazo katika harakati hizi za kutokomeza plastiki ikiwa ni pamoja na ukubali wa watu binafsi kutoona mbadala wa bidhaa hizo.

Image caption Bidhaa za plastiki

Umoja wa mataifa imezitaka kila nchi kuchukua hatua kukabiliana na janga hili la athari za plastiki kwa kupunguza utumiaji wa plastiki.

Miaka kumi iliyopita,BBC iliripoti kuhusu uchafuzi wa bahari ya Pasifiki na namna gani watu wanahitajika kuchukua jitihada za kukabiliana na suala hilo.

Image caption Mwezi mmoja bila kutumia Plastiki

Tafiti zinaonyesha kuwa kama mtu akiamua kuacha kutumia plastiki basi anaweza kuacha hata kwa mwezi mmoja licha ya kwamba miongo kadhaa imepita bila suala hilo kupatiwa ufumbuzi.

Afrika likiwa ni miongoni mwa bara linalokabiliana na tatizo hilo na ufumbuzi wake haijajulikana hatima yake itakuwa lini bado.

Image caption Takataka zinazotokana na plastiki nchini Kenya

Kenya imetoa marufuku ya utumiaji na ununuzi wa plastiki na hata kutoa adhabu kwa watakaokaidi kufuata amri hiyo.

Wakati Tanzania bara licha ya kuweka tangazo kwamba januari mwaka jana ingekuwa tamati ya matumizi ya mifuko ya plastiki lakini utekelezaji wake bado ni mgumu huku kwa upande wa Zanzibar hali imeanza kuwa tofauti kidogo kwa wakazi wa huko kuanza kutumia mifuko ya karatasi.

Matumizi ya plastiki yameonekana zaidi katika ubebaji wa mizigo ;mifuko ya plastiki kuwa mingi na watu hupewa kipindi wanapoenda sokoni kubebea mizigo,vinywaji vya baridi kama soda, maji na juisi vingi vinahifadhiwa katika chupa za plastiki na bidhaa nyingine nyingi zinazohitajika kutumika kwa muda mfupi .

Image caption Vitu 48 vya plastiki unavyoweza kutumia kwa mwezi

Utumiaji wa plastiki ni tabia iliyojengeka kutoka kwa watumiaji na wanunuaji na muda gani uwekwe kuhakikisha matumizi haya ya plastiki yanatokomezwa yaweza kuwa changamoto.

Bidhaa nyingi zimefungwa kwa plastiki,labda sasa unaweza kuwa ni wakati muafaka kwa viwanda kuanza kutengeneza bidhaa za mbadala wake.

Wengine wanasema labda masoko na maduka wakiacha kusambaza bidhaa hizi basi suluhisho linaweza kupatikana.

Image caption Hivi kuna mbadala wa bidhaa za plastiki?

Ni wakati wa kampeni za usafi wa fukwe uwepo katika jamii na wamiliki wa hoteli zilizokuwa karibu na fukwe waweke juhudi zaidi ya usafi wa fukwe zilizoko kwenye ukingo wa hoteli zao.

Aidha gharama ya mbadala wa plastiki yaweza kuwa changamoto na huku wengine ikiwa ni mazoea,hivyo kila serikali inabidi kuliangalia suala hili kwa karibu zaidi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii