Kipchoge aibuka kidedea London Marathon

Eliud Kipchoge mshindi wa kwanza akiwa katikati ,Mshindi wa pili Kitata(Ethiopia) na mshindi wa tatu ni Mo Farah kutoka Uingereza Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eliud Kipchoge mshindi wa kwanza akiwa katikati ,Mshindi wa pili Kitata(Ethiopia) na mshindi wa tatu ni Mo Farah kutoka Uingereza

Mkenya Eliud Kipchoge, aibuka ameibuka kidedea katika mbio za Marathoni za London wa mara ya tatu.

Kipchoge ni moja kati ya wakimbiaji hodari ambae alianza vyema mbio hizo akitumia muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 27.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mo Farah

Mwingereza Mo Farah alikuwa akiongoza katika hatua za awali kabla ya kupoteza mwelekeo na kumaliza katika nafasi ya tatu dakika tano nyuma ya Kipchoge.

Mkiambiaji toka nchini Ethiopia Tola Shura Kitata amemaliza katika nafasi ya pili akiwa nyuma kwa sekunde 33 dhidi ya Kipchoge.

Image caption Vivian Cheruiyot amepata ushindi wake wa kwanza wa London Marathon

Vivian Cheruiyot wa Kenya alishinda kwa upande wa wanawake kwa kutumia muda vizuri katika mashindano.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wakimbiaji zaidi ya elfu arobaini

Wakimbiaji zaidi ya 40,000 walishiriki katika mashindano hayo ya London Marathon katika kipindi cha joto zaidi katika mwaka.