Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwaka huu PFA 2017-18

Mohamed Salah Haki miliki ya picha PA
Image caption Mohamed Salah ndiye mchezaji anayeongoza kwa magoli katika Premier League msimu huu

Mohamed Salah ameshinda tuzo la mchezaji bora la Shirikisho la wacheza soka ya kulipwa mwaka 2017-18.

Mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa Liverpool mwenye umri wa miaka 25, amemshinda Kevin de Bruyne, Harry Kane, Leroy Sane, David Silva na David de Gea katika kura iliyopigwa nwa wachezaji wenzake.

Mchezaji wa Manchester City Leroy Sane ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana , huku naye mchezaji wa Chelsea Fran Kirby ameshinda tuzo ya mchezaji bora mwanamke wa mwaka huu.

Lauren Hemp wa Bristol City ametajwa kama mchezaji bora kijana mwanamke wa mwaka huu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sane played alikuwa na jukumu kuu katika kushinda kwa Manchester City taji la msimu huu

"Ni heshima kubwa na hususan kwamba ni kura iliyopigwa na wachezaji. Naskia raha na sifa kubwa," Salah amesema.

"Sikuapta nafasi nilipokuwa Chelsea. Ni wazi kwamba ningerudi na nionyeshe kila mtu soka yangu. Nadhani niliondoka na nimerudi nikiwa mtu tofuati, na mchezaji tofuati. Naskia raha sana na sifa pia."

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana "furaha ya kuwa na nafasi hiyo " yakuwa meneja wa Salah na kuongeza kwamba ni 'haamini amepata heshima hiyo' ya kushinda tuzo hilo.

Haki miliki ya picha Rex Features

'Kila anachogusa kinaishia wavuni'

Salah amefunga magoli 31 katika mechi 33 kwa timu ya Liverpool iliyo chini ya ukufunzi wa Jurgen Klopp' na anogoza kushinda tuzo la the Golden Boot.

Goli la 31 la raia huyo wa Misri dhidi ya West Brom siku ya Jumamosi lilimueka sawa na Alan Shearer, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez, wanaoshikilia rekodi hiyo kwa mechi ya 38 ya msimu.

Alifunga katika mikondo yote ya mechi ya ilioipa Liverpool ushindi wa 5-1 dhidi ya Manchester City katika robo fainali ya ligi ya mabingwa, pamoja na magoli manne katika ushindi wao wa ligi dhidi ya Watford mnamo Machi.

Huwezi kusikiliza tena
Mohamed Salah ashinda tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika
Mohamed Salah - Msimu wa 2017-18 wa Premier League
Ameshiriki mechi: 33 Mikwaju iliyogusa wavu: 64
Magoli: 31 Dakika alizocheza: 2,657
Amechangia magoli: 9 Nafasi alizotoa: 57
Mikwaju: 132 Pasi alizokamilisha: 684

Ni kwanini De Bruyne alimfuata kwa karibu?

Wengi waliamini ulikuwani ushindani kati ya wachezaji wawili Salah na De Bruyne kushinda tuzo hiyo.

Raia wa Ubelgiji De Bruyne amekuwa na mchango mkubwa katika kampeni ya kushinda taji ya Manchester City.

Ametoa mchango mkubwa (15) na kutoa nafasi za kufunga magoli (104) zaidi ya mchezaji mwingine katika msimu huu wa Premier League this season, pamoja na kufanikiwa kufunga magoli 8.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na City kwa wakati huo rekodi ya thamani kubwa zaidi £ milioni 55 mnamo 2015 na ameshinda taji moja la Premier League na mawili ya League Cups.

Kevin de Bruyne - Msimu wa 2017-18 wa Premier League
Ameshiriki mechi: 34 Mikwaju iliyogusa wavu: 36
Magoli: 8 Dakika alizocheza: 2,836
Amechangia magoli: 15 Nafasi alizotoa: 104
Mikwaju: 84 Pasi alizokamilisha: 2,052
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kevin de Bruyne has created more chances than any other player in the Premier League this season

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuhusu kwanini anaamini De Bruyne angestahili kushinda tuzo hiyo:"Ukiwa unachambua mechi za miezi 9 au 10 basi hakuna mchezaji aliye bora kumliko.

"Kutokana na muendelezo wa kucheza kwake na kucheza siku tatu katika mashindano yote, alikuweko. Samahani pengine kwa takwimu kuna wanaomzidi kwa hilo, lakini hakuna mchezaji katika msimu huu anayeshinda taji mechi tano kabla ya kumalizika, na alikwua bora.

"Nahisi anastahili kulishinda. Lakini mwishowe tutakuwa nyumbani kama mabingwa na ili hilo kutendeka, ni lazima wachezaji wacheze."

Mada zinazohusiana